Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene akipokea wasilisho la mpango wa fursa za uwekezaji katika bonde la Mto Msimbazi na suluhisho la kudumu la mafuriko yanayotokea jijini Dar Es Salaam kutoka kwa Mwakilishi wa DFID Bwana Boshell. Kikao hiko kime fanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mh. Suleiman Jafo wakati wa kikao cha kupokea wasilisho la mpango wa fursa za uwekezaji katika bonde la Mto Msimbazi na suluhisho la kudumu la mafuriko yanayotokea jijini Dar Es Salaam.
Sehemu ya Maafisa wa Serikali kutoka Wizara mbalimbali waliohudhuria katika kikao hiko cha kupokea wasilisho la mpango wa fursa za uwekezaji katika bonde la Mto Msimbazi na suluhisho la kudumu la mafuriko yanayotokea jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mh. Suleiman Jafo akipokea wasilisho la mpango wa fursa za uwekezaji katika bonde la Mto Msimbazi na suluhisho la kudumu la mafuriko yanayotokea jijini Dar Es Salaamkutoka kwa Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Yohannes Kesete. Kikao hiko kilifanyika jijini Dar es Salaam.
……………
Uelewa Zaidi juu ya mradi wa ujenzi wa mto Msimbazi unatakiwa kutolewa ili mradi huo uweze kufanikiwa. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene alipokua akipokea wasilisho la mpango wa fursa za uwekezaji katika bonde la Mto Msimbazi na suluhisho la kudumu la mafuriko katika jiji la Dar es salaam. Kikao hiko kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa TAMISEMI jijini Dar Es Salaam.
“Mradi huu ni muhimu sana na uchambuzi wa kina unahitajika pamoja na uelewa Zaidi ili kuweza kukamilisha mradi huu na kila mmoja anatakiwa kuona umuhimu wa mradi huu” alisema Waziri Simbachawene.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mh. Suleiman Jafo akiongea katika kikao hiko alisema kuwa mradi huo ni fursa ya uwekezaji katika jiji la Dar es Salaam ukifanikiwa basi mandhari ya jiji la Dar Es Salaam itapendeza na kuwa kivutio cha utalii hivyo kulinufaisha Taifa kiuchumi.
Kikao hiko cha kupokea wasilisho la mpango wa fursa za uwekezaji katika bonde la Mto Msimbazi kimeandaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene, ikiwa ni maelekezo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, aliyotoa ili kutafuta suluhu ya kudumu ya mafuriko katika jiji la Dar es Salaam na kuondoa madhara yanayosababishwa na mafuriko.
Mawaziri wengine waliotakiwa kushiriki katika upokeaji wa wasilisho hilo ni Waziri wa fedha na Mipango, Waziri wa Mawasiliano, ujenzi na Uchukuzi, Waziri wa Maji na Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ambao waliwakilishwa na Wawakilishi kutoka Wizara zao.