KAIMU Mkuu wa wilaya ya Muheza Ally Kijazi ambaye pia ni Afisa Tarafa ya Bwembwera wilayani humo akizungumza mara baada ya kufungua Jukwaa hilo la viungo
Afisa Kilimo wilaya ya Muheza Hoyange Mbwambo akizungumza wakati wa Jukwaa hilo
MENEJA wa Benki ya CRDB wilayani Muheza Shija akizungumza wakati wa Jukwaa hilo
Mkulima wa Iliki Kata ya
Zirai Ally Zubeya akichangia jambo kwenye Jukwaa hilo
AFISA Kilimo Idrisa Kijazi akieleza jambo wakati wa Jukwaa hilo
MDAU wa mazao ya viungo wilayani Muheza kutoka Baraza la Biashara za Uholanzi na Afrik akielezea uzoefu wao kwenye Jukwaa hilo
Sehemu ya wakulima wa mazao ya viungo wilayani Muheza wakiwa kwenye kikao hicho
Sehemu ya wakulima wa mazao ya viungo wilayani Muheza wakiwa kwenye kikao hicho
KAIMU Mkuu wa wilaya ya Muheza Ally Kijazi amewaagiza maafisa kilimo na watendaji wa Kata wilayani humo kuhakikisha ndani ya wiki moja washughulikia janga ambalo linaendelea kuathiri zao la pilipili manga ndani ya wiki moja.
Pia alimtaka Afisa Kilimo wa wilaya hiyo Hoyange Mbwambo kushirikiana na maafisa hao kuhakikisha wanapata suluhu ya tatizo hilo ambalo linaleta athari kwa wakulima hao wa pilipili manga.
Kijazi ambaye ni Afisa Tarafa ya Bwembwera wilayani Muheza alitoa agizo hilo wakati wa Jukwaa la wadau wa mazao ya viungo wilayani humo ambapo pia walitumika kuweka mikakati mbalimbali.
Alisema baada ya muda huo waweze kutoa ripoti ya tatizo linalopelekea kukausha zao hilo la pilipili Manga huku likiufanya mti wa zao hilo kukauka na kuleta athari kubwa kwa wakulima.
“Tunaweza kujaribu kufanya tathimini kukuta janga hili ni kubwa hasa kwa wakulima lakini pia mkishindwa kulitatua tupeleke ombi tuweze kusaidiwa kwenye ngazi za juu akiwemo Mkuu wa wilaya hata Mkuu wa Mkoa kuweza kuona namna ya kulitatua kwa pamoja”AlisemaKaimu Mkuu huyo wa wilaya alisema ufunguzi rasmi ya kuvuna zao pilipili Manga wilayani humo litakuwa ni Januari 3 mwakani huku akiwaonya watakaojaribu kuvuna kabla ya muda huo watawachukulia hatua.
“Tunawafahamu njia ambazo mnatumia kusafirisha mazao hayo hivyo hakikisheni mnazingatia muda wa kuvuna msije kuingia matatani kwani watakaokamatwa kabla ya wakati watawashughulikia kwa mujibu wa sheria kukomesha vitendo hivyo “Alisema
Awali akizungumza wakati wa Jukwaa hilo Afisa Kilimo wilaya ya Muheza Hayange Mbwambo alisema kwamba walipokubaliana wawe na muda wa kuvuna iliwasaidia sana kuhakikisha kwenye masoko wanapata pilipili manga iliyokomaa na yenye ubora.
Alisema kwamba licha ya kuwepo kwa kasoro ndogo ndogo zinazungumzika na wamefikia hatua nzuri ya mahali wanapotaka kufika huku akieleza kwamba wameanza kuaminika kwamba asilimia 70 ya pilipili zinazovunwa zinasifa ya ukomavu na kuleta ubora na hivyo kupunguza malalamiko sokoni.
“Lakini pia wiki mbili zilizopita tulitembelewa na wageni kutoka kwenye makampuni ya nje moja ya mambo ambayo walitupongeza ni kuweka utaratibu mzuri wa kufungua msimu”Alisema
Naye kwa upande wake Mkulima wa Iliki Kata ya Zirai Ally Zubeya alisema visababishi vya iliki kuwa changa ni wakulima kuwekeza shamba lake kwa mtu kwamba ukifika muda Fulani atavuna mazao na anapokwenda kuvuna anavuna zote.
Alisema mwarobaini wa suala hilo ni vyama vya ushirika kuhakikisha wanakagua mazao husika yanapokuwa shambani kabla ya kuvunwa kutokana na kwamba nyengine zinavunwa kabla ya kukomaa na kupelekea kukosekana kwa ubora.