Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania Tae Ick Cho akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa wa mkutano wa siku mbili wa Geospatial Information Road Show uliowakutanisha wataalamu wa masuala ya ardhi kutoka nchini Korea na Tanzania unaofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Hamdounny Masour akisoma hotuba katika ufunguzi wa wa mkutano wa siku mbili wa Geospatial Information Road Show uliowakutanisha wataalamu wa masuala ya ardhi kutoka nchini Korea na Tanzania.
Ujumbe wa wataalam kutoka Korea Kusini wakiwa katika mkutano huo.
Ujumbe kutoka Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
Picha zikionesha Mataalam mbalimbali kutoka Korea Kusini na Tanzania wakibadilishana uzoefu kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania Tae Ick Cho amesema Tanzania na Korea Kusini zimekuwa na ushirikiano wa hali ya juu hasa katika masuala ya biashara zilizoruhusu kuvuka mipaka na hiyo yote ni kwa malengo ya kukuza uchumi baina ya nchi hizo mbili.
Amesema Teknolojia bora katika kukuza uchumi ndiyo silaha kubwa na pekee ya kimaendeleo na yenye kuleta ushindani katika soko la dunia na hilo litafanikiwa kamataifa litajikita zaidi katika kuwekeza zaidi katika teknolojia ya sasa ambayo imeteka soko la dunia.
Balozi Tae Ick Cho ameyasema hayo wakati akizungumza katika ufunguzi wa wa mkutano wa siku mbili wa Geospatial Information Road Show uliowakutanisha wataalamu wa masuala ya ardhi kutoka nchini Korea na Tanzania.
Balozi Tae Ick Cho ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa Geospatial Information Road Show malengo makuu ni pamoja na kuendesha semina za kiteknolojia katika usajili ardhi, mikutano ya biashara baina ya Serikali ya Tanzania Makampuni wakilishi ya Korea yaliyopo nchini pamoja na kupeana taarifa mbalimbali katika masuala ya ardhi.
Amesema kuwa ili kuendelea zaidi lazima teknolojia iwe silaha ya kwenda sambamba na maendeleo na bila teknolojia uwezo wa kushindana na mataifa mengine hautakuwepo.
“Matumizi ya teknolojia hasa ICT yana tija sana katika kuyafikia maendeleo na bila hiyo hatutaweza kushindana na mataifa mengine yenye teknolojia ya juu, tukumbuke msemo wa ukiona vyaelea ujue vimeundwa , hivyo hatuwezi kuendelea bila ya kuweka mbele teknolojia, kushirikiana na kuondoa vikwazo” amesema.
Ameongeza kuwa kama ilivyo Korea Kusini lazima watu wajue maeneo yao, ardhi yao na kuitumia katika shughuli za kimaendeleo na kueleza kuwa haba na haba hujaza kibaba hivyo ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili lazima udumishwe zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa upimaji na ramani kutoka Wizara ya Ardhi Hamdounny Masour amesema kupashana habari na kubadilishana uzoefu baina ya kampuni kutoka Korea na Tanzania ni moja katika ya hatua kubwa ambayo itasaidia nchi hizo mbili kufikia malengo.
Masour amesema kuwa kupitia mkutano huo wataendelea kudumisha ushirikiano huo pamoja na kupeana taarifa za kisekta katika masuala ya upimaji wa ardhi.
“Ushirikiano baina ya nchi hizo mbili umekuwa wa kindugu na kupitia Geospatial Information Road Show na Wizara ya Ardhi tutaendelea kupeana taarifa za kisekta ili kuweza kuyafikia maendeleo” ameeleza.
Mkutano huo uliodumu yangu 2013 umewakutanisha wadau kutoka Wizara ya Ardhi nchini pamoja na Wizara ya Ardhi, miundombinu na usafiri kutoka Korea pamoja na wataalamu mbalimbali yakiwemo makampuni makubwa 12 kutoka nchini Korea.