Gavana wa Benki kuu Tanzania Profesa Florens Luoga
GAVANA wa Benki kuu Tanzania Profesa Florens Luoga amesema kuna haja ya kuwa na sera zinazosaidia kukuza sekta ya benki, kuimarisha na kufanya kazi kutokana na mategemeo ya majukumu ya sekta hiyo katika kukuza uchumi wa nchi.
Ametoa kauli hiyo wakati wakufunga mkutano Mkuu wa 19 wa sekta ya fedha nchini mwaka 2019 uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania BoT jijini Dar es Salaam.
Amesema sekta zote nyingine zinapaswa kuielewa vizuri sekta hiyo kwasababu ni rahisi sana kwa sekta za benki husika kuchukuliwa isivyo au kuchukuliwa kama biashara nyingine ya kawaida na kuhusiana nayo katika namna ambayo inaweza usifanye kazi ipasavyo.
Ameongeza kuwa kwa mfano unaweza kukuta kuna mikizano na taasisi zingine za Serikali kama TRA,Polisi,na zingine hata watumiaji wa benki zenyewe wasiwe na mtazamo mzuri ndio maana watu wanaotumia sekta ya Benki ni wachache sana na inaonyesha bado watu hawana uelewa wa kutosha kuhusu sekta hiyo.
“Kwahiyo ni muhimu sasa kupitia mkutano huu wa 19 wa mwaka 2019 wa sekta ya Fedha kuangalia jinsi gani tutajumuisha kila mmoja kila taasisi katika kuielewa sekta ya fedha na kutoa elimu kuhusu utendaji wake na wananchi kujua nini wanapaswa kuelewa wanapotumia Benki.
Akizungumzia majadiliano ya mkutano huo wa siku Mbili wa taasisi za Kifedha Mwenyekiti wa Taasisi za Mabenki nchini (TBA)Abdulmajid Nsekela ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB amefafanua kuwa wametumia Nafasi hiyo kujadili namna ya kupata Fedha ili kusaidia miradi mbambali inayoendelea.
” Tumejadili mengi sana na sehemu ya riba ni moja wapo iliyojadiliwa jinsi gani ya kupata mitaji lakini yenye riba nafuu nakuweza kuwa na upatikanaji wa Fedha zakuweza kutoa kwenye miradi ya muda mrefu nakwamba miradi ya muda mrefu ambayo si ya kimkakati ambayo inachukuwa miaka mingi inapaswa kuwa na riba nafuu ili ilete tija”.amesema Nsekela.
Amessma kwa umoja wao kupitia (TBA) ambacho ni chombo cha usimamizi wa mabenki wamechukuwa hilo na watalifanyia kazi ili wananchi wapate mikopo yenye riba nafuu.pia wamejadili kwa kina namna ya kushirikiana na serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Amefafanua pia wamekubaliana kuwa na sauti ya pamoja ya kupanga malengo yenye muda maalum kuimarisha sekta ya fedha ambapo wamekubaliana kuchambua majadiliano yote na kuunda kamati ndogo ambayo itatoka na mwelekeo ambao watauwasilisha Serikali ili kufanyia kazi.