Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akizungumza na wanafunzi, walimu washule ya Sekondari Twiga iliyopo Kata ya wazo hili leo, alikuwa akizindua na kukabidhi madarasa kwa walimu wa shule leo
……………
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amekabidhi madarasa sita na ofisi tatu za walimu katika Shule ya Sekondari Kigogo iliyopo kwenye Kata hiyo pamoja na Shule ya Sekondari Twiga iliyopo Kata ya Wazo ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wakuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi anakosa nafasi ya kusoma kwa changamoto ya madarasa.
Mhe. Chongolo amezindua madarasa hayo ikiwa ni katika mpango wake wa kujenga madarasa 100 kwakushirikiana na wadau mbalimbali wapenda maendeleo katika Halmshauri hiyo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhe. Chongolo amefafanua kuwa anawapongeza wadau hao walioshirikiana naye katika ujenzi huo kwani madarasa hayo yatasaidia wanafunzi waliomaliza darasa la saba kuendelea na masomo ya Sekondari badala ya kukaa nyumba.
Amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli iliamua kutoa elimu bure kwa kila mmoja ilikuhakikisha kwamba hakuna mtoto anayekaa nyumbani bila kusoma na kwamba atahakikisha madarasa hayo yanajengwa ilikutimiza adhma hiyo.
Amefafanua kuwa kutokana na mpango wa elimu bure uliotolewa na Rais Dk. Magufuli kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wanaosoma hivyo serikali itahakikisha kila mmoja anapata nafasi ya kusoma wakiwa kwenye vymba vya madarasa.
“ Awali tulikuwa na changamoto ya walimu lakini Mhe. Rais amehakikisha kuwa changamoto hiyo imekwisha ,hivi sasa tunachangamoto ya vyumba vya madarasa , hili nalo litakwisha, niwahakikishie serikali ya awamu ya tano ipo pamoja na wananchi wake” amesema Mhe. Chongolo.
Nakuongeza kuwa” leo hii nimekuja mwenyewe kuzindua madarasa haya ili kuona ufanisi uliopo, niseme tu kwamba nimeridhishwa na nimefurahi kuona madarasa haya yamekamilika, sasa imebaki viti na meza ili wanafunzi waweze kusoma nanimeambia tayari vimeshaagizwa.
Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao kwani viongozi wamekuwa wakifanya jitihada zakutosha zakuhakikisha kwamba wanapata madarasa yakusoma.
Mhe. Chongolo amemtolea mfano Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Aron Kagurumjuli kuwa ni kiongozi anayeonyesha katika kuhakikisha kuwa wanafunzi waliopo kwenye Halmashauri yake wanapata madarasa yakusomea ili wote waweze kupata elimu bora.
Mhe. Chongolo amesema kuwa “ kazi nzuri inayofanywa na rais wetu mpendwa ni kuona watu wenye hali ya chini na wale wenye hali ya juu wanapata elimu sawa, kwahiyo niwasihi sana wanafunzi msome kwa juhudi kubwa , wekeni juhudi kwenye masomo yenu, ili msingi tunaowajengea hivi sasa uweze kuimarika.