Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela akipokea msaada kwa ajili ya waathirika wa maafa mkoani humo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, msaada huo umetolewa na ofisi hiyo kupitia Mfuko wa maafa.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Kasongwa akisisitiza umuhimu wa kijiji hicho kuhama katika eneo salama lilioainishwa na wilaya hiyo mara baada ya kupokea msaada vilivyotolewa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Mfuko wa Maafa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko kijijini hapo.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, akisisitiza umuhimu wa kijiji hicho kuhama katika eneo salama lilioainishwa na wilaya hiyo mara baada ya kupokea msaada vilivyotolewa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Mfuko wa Maafa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko kijijini hapo
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mapangoni Kata ya Kerenge Wilayani Korogwe wakifuatilia mkutano wa Mkuu wa wilaya hiyo Kissa Kasongwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe hawapo pichani wakati walipopeleka misaada kwa waathirika wa maafa ya mafuriko kutoka Ofisi ya waziri Mkuu, Mfuko wa maafa
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kisa Kasongwa akipokea msaada kwa ajili ya waathirika wa maafa wilayani humo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, msaada huo umetolewa na ofisi hiyo kupitia Mfuko wa maafa
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mapangoni kilichopo Kata ya Kerenge wakishirikiana na wanajeshi kushusha baadhi ya vitu vya msaada vilivyotolewa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kupitia Mfuko wa Maafa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko kijijini hapo.
************************************
Kamati ya menejineti ya Maafa wilayani Korogwe imeelekezwa kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Mapangoni Kata ya Kerenge Wananchi wa kijiji hicho chenye kaya zaidi ya 250 ambazo ziliridhia kuhama kijiji hicho baada ya baadhi ya nyumba zao kuvunjwa na mawe makubwa yanayoporomoka na maji kutoka milimani na mmomonyoko wa ardhi uliozingirwa na mifereji ya maji, kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha kwa takriban siku 40 mfululizo kijijini hapo.
Akiongea mara baada ya kukagua shughuli za urejeshaji wa hali na kabla ya kukabidhi misaada kutoka Mfuko wa Maafa unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shuhghuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amesema katika menejimenti ya maafa hatua za urejeshaji hali baada ya maafa zinazingatia urejeshaji ulio bora zaidi kuliko wa awali hivyo kwa kuwa kijiji hicho kipo eneo hatarishi wananchi hawanabudi kuishi eneo salama kwa afya zao na mali zao.
“Kwa kuwa utabiri wa hali ya hewa unaonesha mvua za juu ya wastani zitaendelea kunyesha hadi mwanzoni mwa mwakani, niitake Kamati ya maafa ya wilaya kuhakikisha taratibu za kupima maeneo salama kwa wakazi wa kijiji hiki zinakamilika kabla ya mwak huu kuisha ili wakazi wa kijiji hiki waendelee kushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa Taifa” amesisitiza Kanali Matamwe.
Kanali Matamwe ameeleza kuwa kwakuwa serikali imeamua kukihamisha kijiji hicho ili wananchi hao waweze kuishi maeneo salama na wameanza kuwasaidia wananchi hao kupitia Mfuko wa maafa unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, amewataka wadau wengine kuendelea kuwasaidia wananchi hao ili waweze kukamilisha ujenzi wa nyumba bora na salama katika eneo litakalo ainishwa na serikali.
Ofisi ya Waziri Mkuu , Kupitia Mfuko wa Maafa imeikabidhi Kamati ya Menejienti ya Maafa ya Wilaya hiyo misaada kwa kaya zilizoathirika na maafa ya wa mafuriko Wilayani humo ikiwa ni pamoja na magodoro100, bati 200,mikeka 200,blangeti 200,ndoo 200, sleeping bag 100 vikiwa na thamani ya shilingi milioni kumi.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe,
Kissa Kasongwa aliishukuru ofisi ya Waziri Mkuu , Idara ya Uratibu wa maafa kwa
kuona umuhimu wa kuwasaidia waathirika wa mafuriko hayo Wilayani humo
na kwamba mahitaji hayo yemewafikia walengwa kwa wakati muafaka.
“Tumekuwa tukifanya jitihada mbalimbali za kurejesha hali na sasa tayari Kamati ya maafa ya wilaya tumeshaainisha eneo lenye ukubwa wa ekari 150 kwa ajili ya kuanzisha kijiji kipya, lakini nimefuatilia nimeona bado Halmashauri haijaenda kupima eneo hilo, nimemuelekeza mkurugenzi jumatatu hii aende kwenye wnwo hilo nw upimaji uanze mara moja na zoezi hili likamilike ” alisistiza Kasongwa
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Timotheo Mzava alimshukuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, kazi, ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ambaye ana dhamana ya kuratibu maafa nchini kwa kumsikiliza baada ya kuwasilisha matatizo ya wananchi wake na hatimaye kuwatuma wasaisdizi wake kwa ajili ya kushughulikia matatizo hayo ambapo maombi ya wananchi hao yametekelezwa kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa.
Kwa nyakati tofauti wakazi wa kijiji cha Mapangoni Kata ya Kerenge, Aliamini Mrutu na Asha Hizza wameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa misaada waliyowapatia na kubainisha kuwa wako tayari kuhamia katika kijiji kipya kitakacho anzishwa na serikali kwa kuwa wanapoishi sasa maisha yao yako hatarini kw akuwa tayari kaya 63 nyumba zao zimeathirika huku kaya 38 hazina mahala pa kuishi.
Kwa mujibu wa sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha majukumu ya kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika ngazi husika, pamoja na Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji wilaya au mkoa. Pia kutoa taarifa za tahadhari ndani ya eneo husika.