Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi wa eneo la Mpomvu katika kata ya Mtakuja wakati akiwatambulisha Wenyeviti wateule wa CCM.
Katibu wa Mbunge wa Geita mjini, Mariamu Mkaka akitoa ufafanuzi wa jambo katika mkutano wa kuwatambulisha Wenyeviti wateule wa Serikali za mitaa wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Mpomvu kata ya Mtakuja mkiani Geita.
Msanii wa Vichekesho maarufu kwa jina la Kigwendu Kingwendulile akiwaburudisha wananchi waliofika ktika eneo la Mpomvu kwa ajili ya kuwatambulisha wakazi wa eneo la Mpomvu kabka ya Mbunge wa Geita mjini kuzungumza nao.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Benue, James Manakila akiwatambulisha Wajumbe wa mtaa wake kwa Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu.
*****************************
Mbunge wa Geita mjini na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameanza kuwatambulisha Wenyeviti wateule wa Chama cha Mapinduzi( CCM) kwa wananchi kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
Akizungumza na Wananchi wa eneo la Mpomvu katika Kata ya Mtakuja mkoani Geita, Mhe.Kanyasu ametumia fursa hiyo kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika katika kipindi chake cha Uongozi wa miaka minne.
Katika mkutano huo, Mhe.Kanyasu amewatambulisha Wenyeviti wateule wa mitaa saba kwa wananchi na kuwataka watoe ushirikiano ili kuleta maendeleo.
Ametaja mafanikio hayo kuwa yamepatikana katika nyanja ya Elimu, Afya, Barabara, mikopo pamoja na Umeme.
Mbali ya kuelezea mafanikio hayo yaliyopatikana katika utekezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM (2015-2020) katika jimbo hilo, Mhe.Kanyasu ametaka wananchi kutoa ushirikiano kwa Wenyeviti wapya watakaopatikana katika uchaguzi huo ili kuharakisha miradi ya maendeleo.