Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati, Antonio Manyanda, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya Usajili wa Laini za Simu maarufu kama Mnada kwa Mnada lililofanyika mkoani Singida leo.
Afisa Mwandamizi Mawasiliano na Mahusiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mabel Masasi (katikati) akiwaekeza jambo wananchi (hawapo pichani) waliofika kwenye kampeni hiyo iliyofanyika Stendi ya Mabasi ya zamani mjini hapa. Kutoka kulia ni Mchumi Mwandamizi TCRA, Clara Fuko, Afisa Mawasiliano TCRA, Peter Mallundi na Afisa Mawasiliano na Mahusiano TCRA, Judith Shao. Afisa wa NIDA Mkoa wa Singida, Edgar Faraja, akizungumzia mafanikio ya kampeni mkoani humo.
Wakala wa Kampuni ya Simu ya Airtel Mkoa wa Singida, Joseph Petro (kushoto),akitoa huduma ya kusajili laini ya simu kwa Ismail Rashidi katika kampeni hiyo.
Wakala wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Mkoa wa Singida, Violet Kaali, akitoa huduma ya kusajili laini ya simu kwa Bibi Amina Seleman katika kampeni hiyo.
Wakala wa Kampuni ya Simu ya Vodacom, Mkoa wa Singida, Shamimu Abdallah, akitoa huduma ya kusajili laini ya simu kwa njia ya vidole kwa Anna Ntandu katika kampeni hiyo. Katikati ni wakala wa kampuni hiyo, Juma Ntandu.
Wakala wa Kampuni ya Simu ya TTCL, Mkoa wa Singida, Jackline Domonko (kushoto), akitoa huduma ya kusajili laini ya simu kwa njia ya vidole kwa Rose Mayombo katika kampeni hiyo.
Wakala wa Kampuni ya Simu ya TTCL, Mkoa wa Singida, Daniel Joel (katikati), akitoa huduma ya kusajili laini ya simu kwa njia ya vidole kwa Maulid Ramadhani katika kampeni hiyo. Kulia ni Wakala wa Kampuni ya Simu ya TTCL, Mkoa wa Singida, Jackline Domonko.
Afisa wa Wakala wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mkoa wa Singida, Emmanuel Msiru (kushoto), akitoa huduma ya kutoa namba ya Nida, kwa wananchi.
Afisa wa Wakala wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mkoa wa Singida, John Juma, akichukua maelezo kabla ya kumpiga picha Juma Nassoro (kulia).
Afisa wa Wakala wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mkoa wa Singida, Rachel Mazoya (kushoto), akiwaeleza jambo wananchi waliofika kwenye kampeni hiyo.
Afisa wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kutoka Makao Makuu Dar es Salaam, Edna Mgema (kushoto), akitoa huduma ya kutoa namba ya Nida, kwa wananchi.
Wakala wa Kampuni ya Simu ya Halotel, Mkoa wa Singida, Zahara Jumanne (katikati), akitoa huduma ya kusajili laini ya simu kwa njia ya vidole kwa Godlivine Mangi katika kampeni hiyo. Kulia ni Wakala wa Kampuni ya Simu ya Halotel, Mkoa wa Singida, Hamimu Ahmad.
Mkaguzi wa Jeshi la Plosi kutoka Kitengo cha Uhalifu wa Mtandao (Cyber Crime) Makao Makao Makuu Dar es Salaam, Innocent Ndowo (kushoto), akizungumza na mwananchi aliyeibiwa simu.
Mkazi wa Mjini Singida, Omary Kisuke (kulia), akiwaelekeza ndugu zake namna ya kujaza fomu za NIDA.
Wananchi wakisubiri kupiga picha banda la NIDA.
Wananchi wakiwa katika foleni ya kupata huduma banda la NIDA katika kampeni hiyo.
Na Waandishi, Wetu, Singida.
ZOEZI la kusajili laini simu kwa alama za vidole maarufu kama Mnada kwa Mnada linaloratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) limefanikiwa kwa kiasi kikubwa mkoani Singida.
Akielezea zoezi hilo Mkuu wa TCRA Kanda ya Kati, Antonio Manyanda alisema lengo la zoezi hilo ni kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kusajili upya laini zao za simu kwa alama za vidole ambapo lilianzia mkoani Kigoma na baadaye Tabora, Dodoma na kuhitimishwa mkoani Singida kwa Kanda ya Kati.
Manyanda alisema zoezi hilo linashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Jeshi la Polisi kitengo cha uhalifu wa mtandao, makampuni ya simu, uhamiaji pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambapo
lengo ni kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi bora ya mitandao.
“Zoezi hili linafanyika nchi nzima,kwa upande wetu kanda ya kati kwa aana ya Singida, Kigoma,Tabora na Dodoma tunalihitimisha hapa mkoa wa Singida, niwaombe wananchi kujitokeza kwa wingi ili wasajili laini zao”. alisema Manyada.
Kwa upande wake Afisa wa NIDA Mkoa wa Singida, Edgar Faraja alisema wameona ni vyema kusogeza huduma kwa wananchi ili kuhakikisha kila mwananchi anayemiliki laini za simu ifikapo Desemba 31 mwaka huu wawe wamekamilisha usajili wa laini kwa alama za vidole na lengo ni kudhibiti uhalifu wa kimtandao na kuondoa matumizi mabaya ya simu.
Alisema NIDA wamehakikisha kuwasogezea huduma kwa kuwapa namba za utambulisho wananchi katika maeneo wanayoishi na kuwa zoezi hilo linaendea kufanywa kila maeneo ya mkoa huo.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye kampeni hiyo wameshukuru kwa kusongezewa huduma hiyo ambapo awali walikuwa wanaifuata sehemu mmoja tu jambo ambalo lilikuwa linasababisha kuchukua muda mrefu ili mtu apate huduma.