RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli akitunukiwa Shahada ya Heshima ya udaktari wa Falsafa katika fani ya Sayansi ya Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa katika Mahafali ya 10 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dodoma.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli akionyesha Shahada ya Heshima ya udaktari wa Falsafa katika fani ya Sayansi ya Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) mara baada ya kutunukiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa katika Mahafali ya 10 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dodoma.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli akizungumza na Wahitimu wa Kada mbalimbali katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya udaktari wa Falsafa katika fani ya Sayansi ya Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) katika Mahafali ya 10 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Wahitimu wa uuguzi wakila kiapo mara baada ya kutunukiwa Shahada katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika Mahafali ya 10 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Wahitimu wa kada mbalimbali wa Chuo cha Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa wanasubiri kutunikiwa na Mkuu wa Chuo hicho Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa katika Mahafali ya 10 ya chuo hicho.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli,akishuhudia baadhi ya wahitimu wakitunukiwa shahada mbalimbali na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa katika Mahafali ya 10 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dodoma.
Spika Mhe.Job Ndugai,akiteta jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,ambao walihudhuria Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli ametunukiwa Shahada ya Heshima ya udaktari wa Falsafa katika fani ya Sayansi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli ametunukiwa Shahada ya Heshima ya udaktari wa Falsafa katika fani ya Sayansi.
Picha na Alex Sonna-Fullshangwe blog
………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli ameviagiza Vyuo Vikuu Nchini kufanya tafiti mbalimbali kwa kutumia wataalam wa ndani kulingana na mahitaji na vipaumbele vya nchi kwa kupunguza kutegemea misaada ya nje katika tafiti zao.
Hayo ameyasema leo wakati akitunukiwa Shahada ya Heshima ya udaktari wa Falsafa katika fani ya Sayansi ya Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) katika mahafali ya 10 ya chuo hicho.
Mhe.Magufuli amewataka wataalam kuacha kutegemea misaada kutoka nje ya nchi hivyo ni wakati wakutengeneza tafiti zao kwasabau wanaotoa misaada ndio wanaowapa ajenda ya kutafiti.
Mara baada ya kutunukiwa shahada hiyo,Rais amekishukuru chuo kikuu cha Dodoma kwa kumtunikia shahada hiyo ambayo itakuwa ya pili ya uzanifu, baada ya kupata shahada yake ya kwanza ya uzanifu katika Chuo Kikuu cha Dar es Slaam(UDSM) iliyohusu utafiti maganda ya korosho yanavyoweza kuzuia kutu.
“Niwashukuru sana mmeniambia nimekuwa mtu wa Tatu kutunukiwa shahada ya heshima kwa kutanguliwa na watangulizi wangu, ambao ni Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete na Komredi Mfalme Rashid Kawawa ambao walitunukiwa shahada hizo mwaka 2010,”amesema Mhe.Magufuli
DKt.Magufuli amesema kuwa wanafunzi takribani 6,488 wametunukiwa shahada mbalimbali, na hivyo bila shaka shahada mnazotunukiwa ni matokeo ya jitihada, bidii zenu na nidhamu kubwa mliyoionyesha wakati wa masomo yanu, nimatumaini kuwa mtatumia elimu mliyoipata kuchangia maendeleo ya nchi.
Amevitaka Vyuo Vikuu nchini kote kuanza kubadili muelekeo wa kuwa viwanda vya kuzalisha watumishi wa umma badala yake wawatayarishe wahitimu wa kuweza kujiajiri wenyewe.
“Tengenezeni agenda za utafiti zenye kutatua matatizo na kukidhi mahitaji ya ajenda zetu wenyewe, ili kukuza uwezo wa kujitegemea katika gharama za utafiti, anzisheni na imarisheni kutafuteni njia mbalimbali za kuimarisha tafiti zenu za fedha ikiwemo kutumia taaluma zenu.
Mhe.Magufuli amesema kuwa tafiti na matokeo ya tafiti hizo zitakuwa na maana ikiwa zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watanzania, angalieni namna tafiti zenu zinavyoweza kusaidia utekelezaji na kukabiliana na changamoto mbalimbali ya dira ya maendeleo ya taifa.
Aidha amewataka kubainisha matatizo na kutafuta majibu yanayowakabili wazalishaji mbalimbali kama, vile wakulima, wafugaji, wachimbaji wa madini, wavuvi na wenye viwanda
“Vyuo vyetu lazima viwe chimbuko la maarifa mapya na chachu ya maendeleo, haitasaidia kama matokeo ya tafiti, maarifa na ujuzi na mbinu zinazozalishwa katika vyuo havitatumiwa na wao wenyewe ndio mana kupitia serikali anayoiongoza wamejitahidi sana kutumia wataalam wao wa ndani”
Rais Magufuli ametoa wito kwa serikali na taasisi zote za umma kutumia wataalam wa ndani, kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanajiongezea uwezo wa kujitegemea, uzalishaji, maarifa na utaalam na hiyo itawaongezea uwezo wao wa kujitegemea katika nyanja mbalimbali na katika maendeleo ya nchi yao.
Pia amewataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kuchangia maendeleo ya nchi, “nimefurahi kusikia baada ya wiki moja mtakuwa mmepata vyetu vyenu, na hilo lifanyike ili mkavitumie kuchangamkia ajira na kama zipo wengine waweze kuzipata na wengine wakajiajiri pia.
Awali, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Gaudencia Kabaka amesema kuw wameanzisha kitengo kipya chuoni hapo chenye lengo la kuongeza tija na ufanisi katika kazi kwa taasisi mbalimbali na kupunguza gharama zisizo na tija.
Mhe.Kabka amesema kuwa baraza la chuo lilifanya mabadiliko ya kimuundo ambapo walifuta sifuri zote zilizokuwepo 15, baadhi ya idara na kuunganisha idara zilizokuwa ndogo
“Idara zimepungua kutoka 62 hadi 30 pia tumeanzisha vitengo na lengo la mabadiliko haya ni kutokana na agizo la Serikali kwa wizara, idara na wakala wa serikali kupitia miiko ya uendeshaji katika taasisi mbalimbali nchini,”amesisitiza Mhe.Kabaka
Aidha amefafanua kuwa lengo ni kuongeza tija na ufanisi katika kazi na kupunguza gharama zisizokuwa na tija.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Faustine Bee amesema kuwa wameshafanya uhakiki wa taaluma za watumishi wa chuo hicho na wale wasio na sifa majina yao yatapelekwa ofisi ya utumishi ili wapangiwe kazi nyingine.
Hata hivyo ameongeza kuwa kumeibuka tabia ya baadhi ya watendaji wa vyuo mbalimbali nchini hususani chuo hicho kuwanyanyasa wanafunzi kijinsia lkwa kuomba rushwa ya ngono ili wawafaulishe ambapo kamati imeundwa kuchunguza hilo na watakaobainika watachukuliwa hatua.