Home Mchanganyiko KAGERA YAONGOZA KUWA NA IDADI KUBWA YA UKATILI WA KIJINSIA

KAGERA YAONGOZA KUWA NA IDADI KUBWA YA UKATILI WA KIJINSIA

0

Na Silvia Mchuruza,Kagera.

Mkoa Wa kagera unaongoza kuwa na idadi kubwa ya ukatili Wa kijinsia katika jamii ikiwa ni utafiti uliofanywa na muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama kwa kushirikiana na UN WOMEN  katika kufuatilia upigaji vita ukatili Wa kijinsia.
Hayo yamesemwa na Afisa mradi wa utepe mweupe Wa uzazi salama Bw.Datus Ng’wanangwa unaojihusisha zaidi kupinga ukatili Wa kijinsia ikihusisha wilaya tatu za Mkoa Wa kagera ambazo ni wilaya ya muleba,halmashauri ya bukoba vijijini pamoja na bukoba manispaa.
Hata hivyo nae Afisa ustawi Mkoa Bi.Rebeccah Guambara amesema kuwa kama Mkoa unaendelea kutoa elimu hasa kwa viongozi Wa kijamii ambao wapo katika jamii za wananchi kila siku.
“Watu ambao wanakumbwa zaidi na changamoto kubwa ya ukatili Wa kijinsia ni wanawake na watoto hivyo tunajitaidi kutoa mafunzo ya uelewa kwa makundi mbalimbali hili kuepukana na changamoto  hizi na hata kuipa uelewa jamii kwa ujumla”
Sambamba na hayo ameongeza kuwa ukatili ni kitu kinachoweza kumfanya mtu kupata madhara ya kunyanyapaliwa na jamii kutokana na kutopata elimu ya kutosha kuhusu vitendo hivyo ambapo mradi Wa utepe mweupe utasaidia zaidi kutoa elimu katika jamii kupitia wilaya hizo tatu za Mkoa.