Mratibu wa Mtandao TECMN, Bw.Michael Sungusia akiongea na Wanahabari katika Mkutano uliowahusisha wadau mbalimbali wanaohusika na kuktetea haki za Mtoto nchini Baadhi ya wadau mbalimbali wa wanaohusika na utetezi wa haki za Mtoto nchini wakifuatilia mkutano
****************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Mahakama katika shauri la Rebeca Gyumi iliamuru Serikali kufanya marekebisho ya sheria ndani ya mwaka mmoja na kusahihisha vifungu vya kibaguzi vya 13 na 17 na kuweka miaka 18 kama umri wa chini unaostahili kwa ndoa kwa wavulana na wasichana.
Ameyasema hayo leo Mratibu wa Mtandao TECMN Bw.Michael Sungusia katika mkutano uliwakutanaisha wadau mbalimbali kutoa tamko kutokomeza ndoa za utotoni Tanzania kupongeza uamuzi wa Mahakama ya rufani ya Tanzania kuhusu mabadiliko ya sheria ya ndoa 1971.
Akizungumza katika mkutano huo, Bw.Sungusia amesema kuwa shauri la Rebeca Gyumi ni ushindi wa kipekee kwa watoto wa kike wa Tanzania.Linaonesha kwamba wanawake wanapaswa kuwa na haki ya kuridhia kuolewa na kwamba, umri wa chini wa kuolewa/kuoa lazima uwe na miaka 18 kwa mwanamke na mwanaume.
“Shauri la Rebeca Gyumi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali katika shauri la madai Na.5 ya 2016 lilipinga uhalali wa kikatiba wa ndoa za utotoni.Matokeo yake ni kwamba Mahakama Kuu Tanzania ilitamka kwamba vifungu vya 13 na 17 vya sheria ya ndoa ni vya kibaguzi na vinakwenda kinyume na katiba”. Amesema Bw.Sungusia.
Pamoja na hayo Bw.Singusia amesema kuwa kwa wastani kati ya watoto watano wakike wawili huolewa kabla ya umri wa miaka 18. Utafiti wa Kidemografia na afya (TDHS 2015)unaonesha kuwa asilimia 31 ya wanawake kati ya umri wa miaka 20-24 waliolewa wakiwa na umri wa chini ya m iaka 18.
Aidha, Bw.Singusia ameeleza kuwa ndoa za utotoni kwa hapa Tanzania huathiri zaidi watoto wa kike kwani kwa wastani wanawake wengi huolewa mapema zaidi kwa tofauti ya umri wa miaka 5 wakilinganishwa na wanaume.