Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Tabora wakishiriki mazoezi ya kukimbia jana ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha uzinduzi wa wiki ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukizwa.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala (aliyekaa) akipima Shinikizo la Damu jana ikiwa ni sehemu ya kushiriki uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukizwa kwa Mkoa wa Tabora.
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Tabora wakishiriki mazoezi ya viuongo jana ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha uzinduzi wa wiki ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukizwa.
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Tabora wakisikiliza mada mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha uzinduzi wa wiki ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukizwa kwa Mkoa wa Tabora jana.
Katibu Tawala Msaidizi (Afya) Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatinisibwa akitoa taarifa kuhusu ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa Mkoa wa Tabora jana ikiwa ni sehemu ya wiki ya maadhimisho ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa hayo.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Hamis Mkunga akitoa salamu za Mkoa jana wakati wa wiki ya maadhimisho ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala akizundua jana wiki ya maadhimisho ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza kwa Mkoa wa Tabora.
………………….
NA TIGANYA VINCENT
IDARA ya Afya Mkoani Tabora imesema kuwa jitihada za makusudi zinahitajika kuzuia na kudhibiti ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza mkaoni humo.
Baadhi ya magonjwa yasiyoambukizwa ni kisukari, shinikizo la damu, seli mundu, saratani , magonjwa ya akili na pumu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni wa kuzuia na kudhibiti magonjwa hayo Katibu Tawala Msaidizi (Afya) Dkt. Honoratha Rutatinisibwa alisema toka mwaka 2017 hadi 2019 kumekuwepo na ongezeko la magonjwa hayo Mkoani humo.
Alitaja baadhi ya wagonjwa wa magonjwa yasioambukizwa waliongeza kuwa ni kisukari ambapo mwaka 2017 walikuwa 4,345 na kuongezaka hadi kufikia 6,732 mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la wagonjwa 2,387 sawa na asilimia 35.
Dkt. Rutatinisibwa alisema kwa upande ugonjwa wa Shikizo la Damu, wagonjwa wameongezeka katika kipindi hicho hicho kutoka 13,940 hadi kufikia 19,460 ikiwa ni ongezeko wagonjwa 5,520 sawa na asilimia 28.
Aliongeza kuwa upande wa ugonjwa wa pumu umeongezeka kutoka wagonjwa 5,338 hadi kufikia wagonjwa 8,434 ikiwa kuna ongezeko la wagonjwa 3,096 sawa na asilimia 37 ndani ya kipindi hicho hicho.
Akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya maadhimisho ya Kapambana na magonjwa hayo ,Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala aliwataka wakazi wa Mkoa wa Tabora kujenga tabia ya kuchunguza afya zao mapema walau mara mbili kwa mwaka.
Alisema hatua hiyo itasaidia kugundua matatizo mapema na kuwahi kukabiliana nalo likiwa bado katika hatua za awali kwa kutumia gharama kidogo.