Home Mchanganyiko MILIONI 254 ZAKAMILISHA MAKAZI YA FAMILIA SITA ZA ASKARI MKOANI TABORA

MILIONI 254 ZAKAMILISHA MAKAZI YA FAMILIA SITA ZA ASKARI MKOANI TABORA

0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora (RPC) Barnabas Mwakalukwa akitoa salama Jeshi hilo jana wakati wa uzinduzi wa nyumba mpya za makazi mapya ya Askari mjini Tabora.

Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tabora (Serikali za Mitaa) Nathalis Linuma akitoa salamu za Mkoa jana wakati wa sherehe fupi ya  uzinduzi wa nyumba mpya Askari mjini Tabora.

Baadhi ya Maaskati na Wageni waalikwa walioshiriki uzinduzi wa nyumba mpya za makazi ya askari jana mjini Tabora
 
Picha na Tiganya Vincent

………………..

NA TIGANYA VINCENT

MAJENGO matatu ya makazi mapya ya Polisi yamegharimu jumla ya shilingi milioni 254 kukamilika zikiwemo zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na wadau Mkoani Tabora.

Akisoma risala wakati wa uzinduzi wa majengo hayo Marakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Msabila Kulwa Bundala alisema kila jengo lina nyumba mbili za makazi ambalo kila moja limegharimu shilingi milioni 84.6.

Alisema katika kiasi cha fedha cha shilingi bilioni 10 , Mkoa wa Tabora ulipata shilingi milioni 150 ambapo wadau wa Jeshi hilo walichangia zaidi ya milioni 100.

Bundala  alisema michango ya wadau ilijumuisha fedha tasimu , saruji , vifaa vya umeme na maji.

Naye Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tabora (Serikali za Mitaa) Nathalis Linuma alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuboresha makazi ili wawe na mazingira mazuri ya kuishi na kutoa huduma nzuri kwa jamii.

Alisema maendeleo hayana mwisho ni vema utaratibu wa jamii kushirikiana na Polisi kuboresha mazingira ya kuishi na kufanyia kazi yakaendelea ili kuwawezesha kuishi sehemu moja ambayo itakuwa rahisi kuisaidia jamii pindi wanapohitajika.

Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Barnabas Mwakalukwa   alitoa wito kwa wadau mbalimbali Mkoani Tabora kusaidia kukamilisha majengo ya Ofisi likiwemo la Asakari wa Usalama barabarani ambayo yalianza kujengwa mwaka 2015 ambayo yamesimama.

Alisema uwepo wa Ofisi ya za kutosha utaongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa kuwa na mazingira mazuri ya kutoa huduma kwa wananchi mbalimbali.