Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora (RPC) Barnabas Mwakalukwa akitoa salama Jeshi hilo jana wakati wa uzinduzi wa nyumba mpya za makazi mapya ya Askari mjini Tabora.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tabora (Serikali za Mitaa) Nathalis Linuma akitoa salamu za Mkoa jana wakati wa sherehe fupi ya uzinduzi wa nyumba mpya Askari mjini Tabora.
………………..
NA TIGANYA VINCENT
MAJENGO matatu ya makazi mapya ya Polisi yamegharimu jumla ya shilingi milioni 254 kukamilika zikiwemo zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na wadau Mkoani Tabora.
Akisoma risala wakati wa uzinduzi wa majengo hayo Marakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Msabila Kulwa Bundala alisema kila jengo lina nyumba mbili za makazi ambalo kila moja limegharimu shilingi milioni 84.6.
Alisema katika kiasi cha fedha cha shilingi bilioni 10 , Mkoa wa Tabora ulipata shilingi milioni 150 ambapo wadau wa Jeshi hilo walichangia zaidi ya milioni 100.
Naye Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tabora (Serikali za Mitaa) Nathalis Linuma alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuboresha makazi ili wawe na mazingira mazuri ya kuishi na kutoa huduma nzuri kwa jamii.
Alisema maendeleo hayana mwisho ni vema utaratibu wa jamii kushirikiana na Polisi kuboresha mazingira ya kuishi na kufanyia kazi yakaendelea ili kuwawezesha kuishi sehemu moja ambayo itakuwa rahisi kuisaidia jamii pindi wanapohitajika.
Alisema uwepo wa Ofisi ya za kutosha utaongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa kuwa na mazingira mazuri ya kutoa huduma kwa wananchi mbalimbali.