NA MWANDISHI WETU, KISARAWE
KATIKA hali isiyo ya kawaida, idadi kubwa ya wanawake wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani wamejitokeza
kujisajili Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) hatimaye watambulike kama walipakodi na waweze kufanya biashara
zao kwa uhuru na halali.
kujisajili Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) hatimaye watambulike kama walipakodi na waweze kufanya biashara
zao kwa uhuru na halali.
Hali hiyo ilijitokeza wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma, elimu ya kodi na usajili wa walipakodi inayoendelea katika mkoa wa Pwani ambapo katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji idadi kubwa ya wanaume ndiyo iliyokuwa inajitokeza kupata TIN lakini hali imekuwa tofauti katika Wilaya ya Kisarawe ambapo idadi kubwa ya wanawake ndiyo iliyojitokeza.
Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi kutoka TRA, Honesta Ndunguru amesema ni kweli kwamba idadi kubwa ya wanawake wamejitokeza kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi
katika Wilaya ya Kisarawe ukilinganisa na wilaya zingine za mkoa wa Pwani walikopita.
katika Wilaya ya Kisarawe ukilinganisa na wilaya zingine za mkoa wa Pwani walikopita.
Ndunguru amesema, TRA imevutiwa na mwamko wa wananchi wa wilaya zote katika mkoa wa Pwani na kuwapongeza wale wote waliojitokeza kupata huduma, elimu pamoja na kujisajili kuwa walipakodi.
“Kwa mwitikio huu, inadhihirisha kwamba elimu ya kodi tunayoitoa inawafikia walengwa na wanafuata sheria ya kodi inayomtaka kila mfanyabiashara kujisajili na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi inayotolewa bure na TRA”, amesema Ndunguru.
Kwa mujibu wa Ndunguru kati ya wananchi 10 waliojitokeza kupata TIN 8 kati yao walikuwa wanawake, tofauti na wilaya nyingine ambapo idadi kubwa walikuwa wanaume.
Baadhi ya wanawake waliojitokeza katika viwanja vya stendi ya zamani ili kusajiliwa na kupata TIN hawakusita kueleza hisia zao ya kwamba wanawake wa wilaya ya Kisarawe wamepata mwamko wa kufuata sheria za nchi zikiwemo za kulipa kodi ili
waweze kutumia fursa mbalimbali ambazo zionatokana na kutambulika na serikali kama vile kupata mikopo ya wajasiliamali na huduma zingine muhimu.
waweze kutumia fursa mbalimbali ambazo zionatokana na kutambulika na serikali kama vile kupata mikopo ya wajasiliamali na huduma zingine muhimu.
“Binafsi nimehamasika na kuja kupata Tin kwa sababu nimeelimishwa na maofisa wa TRA na nimeelewa umuhimu wa kujisajili kama mlipakodi na kulipa kodi kwa nchi yangu”,
amesema Fatma Omari
amesema Fatma Omari
Naye Sophia Ndume mkazi wa Kisarawe ameongeza kuwa wanawake wa Kisarawe ni wahangaikaji katika biashara ndiyo maana wamehamasika kwa wingi kuja kuchukua
TIN ili wakafanya biashara zao kwa uhuru bila kubughudhiwa.
TIN ili wakafanya biashara zao kwa uhuru bila kubughudhiwa.
Zainess Madeng’ha ambaye ni mmiliki wa saluni ya kike, amesema amehamasika kuchukua TIN baada ya kupata elimu kutoka kwa maofisa wa TRA na kwamba huduma hiyo imesogezwa karibu na inapatikana bure.
“Kwa kweli nimeona nitumie fursa hii kwa kuwa huduma imenifuata dukani kwangu na vile vile Napata huduma hii bure bila kulipia chochote”, alisema.
TRA inafanya wiki ya elimu kwa mlipakodi katika mikoa ya Pwani na Morogoro kwa lengo la kusogeza huduma za ulipaji kodi karibu na wananchi lakini pia kusajili
walipakodi ili kuongeza idada ya walipakodi nchini.
walipakodi ili kuongeza idada ya walipakodi nchini.
Zainess Madeng’ha (kulia), mkazi wa Kisarawe mkoani Pwani akifurahia kupokea Cheti cha Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kutoka kwa maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika wiki ya mlipakodi inayoendelea mkoa wa Pwani.
Afisa wa TRA akiwahudumia akina mama hawa kupata Vyeti vya Utambulisho wa Mlipa kodi yaani TIN, huko Kisarawe mkoani Pwani.
Wanawake wa wilaya ya Kisarawe wakichangamkia fursa ya kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN)