Wafugaji kote nchini wametakiwa kutumia njia ya Uhimilishaji/upandishaji mbegu za ng’ombe kwa njia ya kisasa ili kuweza kupata mbegu nzuri na za kisasa kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Animal Breading East Africa (ABEA) Bw. Masele Hussein katika mkutano na waandishi wa habari uliyofanyika Ocean Drive Masaki jijini Dar es salaam Novemba 14, 2019.
Bw. Masele amesema kuwa njia hii ya kupandisha mbegu bandia za ng’ombe (Artificial Insemination) inafaida kubwa sana kwa mfugaji kwa kuwa ng’ombe wanaozaliwa katika njia hii wanakuwa na nyama nyingi, wanatoa maziwa ya kutosha pia wanakuwa imara dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Aidha amesema kuwa kwa wastani ng’ombe hutoa zaidi ya mbegu milioni tano na matokeo yake anazaliwa ndama mmoja hii inamaanisha kuwa kuna mbegu nyingi zinapotea bure, lakini kwa njia hii mfugaji anaweza kupata ndama hata zaidi ya mia moja, pia hata akiwa ananyonyesha anakuwa na uwezo wa kupandikiziwa mbegu nyingine.
Ameendelea kusema kuwa kwa ufugaji wa dume ni hasara kutokana kuwa dume moja linakula chakula mala mbili zaidi ya jike, na dume lenyewe kazi yake ni moja tu ya kuzalisha ni bora kuwa na majike ambayo yataleta faida kubwa kupitia mfumo huu kuachana na madume kabisa.
Ameongeza kuwa kwa njia hii ya kupandikiza mbegu za n’gombe haijaanza hivi karibuni ilikuwepo toka enzi za ukoloni ila kwa sasa ndiyo imeshika kasi kubwa hapa nchini kwetu na kuongeza kuwa njia hii inafanya kazi vizuri sana na mpaka sasa mikoa takribani 9 wameweza kuifikia ikiwemo Kagera, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya, Iringa, Njombe pamoja na makao makuu Dar es salaam.
Bw. Masele ameendela kusema kuwa Land 0, Lakes Venture 37 wakiwa kama wasimamizi wa mradi huo, kwa kushirikiana na ABEA ambao ni watekelezaji pamoja na kituo cha Uhimilishaji cha Taifa (NAIC) kilichopo Usariva jijini Arusha ambapo kwa sasa wana madume 11 kutoka Switzerland pamoja na South Africa kwa ajili ya kutoa mbegu zilizo bora kwa wafugaji wa hapa nchini.
Amesisitiza kuwa njia hii ya Uhimilishaji (AI) inawasaidia wafugaji kupata makabila tofautitofauti ya ng’ombe kutokana na kuwa mbegu hizi zinakusanywa kutoka kwa madume mbalimbali ambayo yamethibitishwa kuwa na mbegu nzuri na zenye taarifa za kutosha kuhusu uzalishaji, lakini pia njia hii inaepusha kupata mbegu za ukoo mmoja kwa kuwa dume linaweza baadae kuja kumpanda hata mtoto wake kitu ambacho siyo kizuri.
Ameongeza kwa kusema kuwa inasaidia kuwaepusha ng’ombe na magonjwa mbalimbali ya kizazi tofauti na njia ya asili ambapo dume moja linapanda majike tofautitofauti hivyo linaweza kuwaambukiza magonjwa ng’ombe wengine endapo litakuwa nao au litapata kwa mmoja wa majike hayo na kuendelea kusambaza kwa wengine.
kawaida.