Home Mchanganyiko MAKOSA 2,032 YA BARABARANI NA UKIUKWAJI SHERIA YAMERIPOTIWA VITUO VYA POLISI KWA...

MAKOSA 2,032 YA BARABARANI NA UKIUKWAJI SHERIA YAMERIPOTIWA VITUO VYA POLISI KWA MWEZI WA OKTOBA 2019

0

Mtakwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Kitengo cha Takwimu za makosa ya Jinai madai na jinsia Asha Mussa Mahfoudh akitoa takwimu za makosa ya barabarani ambapo imeonekanwa kupanda kutoka ajali 22 kwa mwezi wa Oktoba 2018 hadi ajali 32 kwa mwezi wa Oktoba 2019, hafla iliyofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar.

Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria katika Mkutano kuhusiana na utoaji wa takwimu za ajali ambapo imeonekanwa kupanda kutoka ajali 22 kwa mwezi wa Oktoba 2018 hadi ajali 32 kwa mwezi wa Oktoba 2019.

Mkuu wa Kitengo cha takwimu za uhalifu makao makuu ya Polisi Zanzibar Ispekta Khamis Mwinyi Bakari (katikati) akijibu maswali yaliyoulizwa na Waandishi katika mkutano wa utoaji wa takwimu za makosa ya ajali za Barabarani ambapo imeonekana kupanda kutoka ajali 22 kwa mwezi wa Oktoba 2018 hadi ajali 32 kwa mwezi wa Oktoba 2019 sawa na asilimia 45 .5, hafla iliyofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar.

Picha na Yussuf Simai – Maelezo Zanzibar.

………………………………………..

Na Mwashungi Tahir,Maelezo     

Jumla ya makosa  2,032 ya  makosa ya  barabarani pamoja na ukiukwaji wa sheria  yameripotiwa  katika vituo mbali mbali vya polisi kwa mwezi wa Oktoba 2019 mwaka huu.

Hayo aliyasema Mtakwimu Mkuu wa Serikali kwenye kitengo cha takwimu za makosa ya Jinai ,Madai na jinsia  Asha Mussa Mahfoudh wakati akizungumza na waandishi wa habari  huko katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Mazizini .

Amesema idadi ya ajali  barabarani  kwa mwaka uliopita zimeongezeka kutoka ajali 22 kwa mwezi wa Oktoba , 2018 hadi 32 mwezi wa Oktoba , 2019 sawa na 45.5.

Akizungumza kuhusu ajali za barabarani Afisa huyo amesema jumla ya ajali 32   zimeripotiwa kutokea mwezi wa Oktoba mwaka huu  ambapo waliofariki  ni 19   na waliojeruhiwa ni 33.

Kwa upande wa  ukiukwaji wa sheria wa makosa ya  barabarani  , Magharibi A na Magharibi B zimeongoza zaidi kwa makosa ya kushindwa kuvaa sare na beji kwa Tingo na Madereva wa gari za abiria, kutofuata miongozo na kanuni za usalama barabarani.

 Alisema  makosa mengine  ni  kuendesha vyombo vya moto ikiwemo    gari,vespa,pikipiki na fifti  bila ya leseni  wala bima na kukosa  kuvaa helmet pamoja na kuzidisha idadi ya abiria na mizigo.

Nae Inspekta Khamis Mwinyi Bakari kutoka Kitengo cha Takwimu za  uhalifu kutoka Makao Makuu ya Polisi amewataka madereva kuwa makini wanapokuwa barabarani ili kupunguza ajali kutokana na ubovu wa barabara .

Kwa upande wa Koplo Khamis Juma kutoka Ofisi ya Mkuu wa kikosi cha usalama wa barabarani  amesema ongezeko la ajali barabarani katika Wilaya ya Magharibi A linatokana na ubovu wa barabara ikiwemo njia ya Bububu kwa kisasi na mshelishelini  hivyo amewataka madereva kuwa waangalifu ili waweze kupungua ajali za kizembe