Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Rafiki wa Mazingira (TAPAFE), Mhe. Jitu Soni akitoa maelezo ya utanguzili kuhusiana na Mpango Kazi wa chama hicho kwa Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai kabla ya kuuzindua rasmi mpango huo katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akifuatilia uwasilishwaji wa mada katika Mkutano wa Chama cha Wabunge Rafiki wa Mazingira (TAPAFE), katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Pembeni yake ni Mwenyekiti wa chama hicho Mhe. Jitu Soni.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akifungua Mpango Kazi wa Chama cha Wabunge Rafiki wa Mazingira (TAPAFE), katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa chama hicho Mhe. Jitu Soni na Florentina Julius kutoka Jumuiko la Maliasili Tanzania.