UTAWALA BORA
DODOMA , Nov 13,2019
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi (
AG)leo ( jumatano) amekutana na kisha kuwa na mazungumzo na
Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Mazungumzo baina ya AG na Tume hiyo ambayo iliongozwa na
Mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Mhe. Methew Mwaimu yamefanyika
katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyopo katika
Mji wa Kiserikali Mtumba Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe. Jaji Mstaafu Methew Mwaimu
alimueleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwamba, Madhumuni ya
ziara hiyo pamoja na masuala mengine, yalikuwa ni
kujitambulisha kwake lakini pia kujadiliana na
kubadilishana mawazo ya namna Ofisi hizo mbili zinaweza
kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kwa upande wake Profesa Kilangi, aliishukuru Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala bora wa kuona umuhimu wa kumtembelea na
kubadilishana naye mawazo ikiwa ni muda mfupi tangu
kuteuliwa kwao na kuapishwa kwao.
G ameihahidi tume hiyo ushirikiano madhubuti kutoka katika
Ofisi yake.
Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Dkt. Evaristo Longopa na Mkurugenzi wa Idara ya
Uratibu na Huduma za Kisheria, Dkt. Gift Kweka.
Itakumbukwa kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora Mhe. Jaji Mstaafu Methew Mwaimu na Makamisha wake
waliteuliwa Mwezi Septemba mwaka huu na Mhe. Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.