Home Mchanganyiko WATATU MBARONI KWA TUHUMA ZA WIZI WA COMPUTER 23

WATATU MBARONI KWA TUHUMA ZA WIZI WA COMPUTER 23

0

****************************

NA FARIDA SAIDY MOROGORO

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Morogoro Linawashikilia Watuhumiwa
Watatu Kwa Kosa La Kuvunja Moja Ya Ofisi Za Shule ya msingi
msamvu B iliyoko kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro
Majira Ya Usiku Na Kuiba Computer 23.

Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Kamanda Wa Polisi Mkoa wa
Mororgoro Willibroard Mutafungwa Amesema Tukio Hilo Limetokea
Manamo Tar 11 Mwezi Novemba Mwaka Huu Katika Shule Hiyo ndani
ya Chumba Kilicho Na Computer Hizo Kisha Kuzibeba Kwenye Viroba
Na Kuzipakia Kwenye Gari Isiyofahamika Na Kutoweka Nazo Kusiko
Julikana.

Kamanda Mutafungwa Amesema Watuhumiwa Wote Watatu
Wamehojiwa Na Kukiri Kutenda Kosa Hilo Na Uchunguzi Zaidi
Unaendelea Kuwabaini Watuhumiwa Wote Walioshirikiana Nao
Akiwemo Mlinzi Wa Shule Hiyo Ambaye Amekimbia Baada Ya Tukio
Hilo.

Kwa Upande Wa Mwalimu Mkuu Wa Shule Hiyo Bwa Elidalimetusi
Selemani Likomba Amelishukuru Jeshi La Polisi Kwa Jitihada
Walizofanya Mpaka Kufanikiwa Kuzipata Computer Hizo huku
Mwanafunzi Wa shule hiyo Bi Mwajuma Ramadhani amesema
amesikitishwa Na kitendo cha kuiibiwa kwa Kompyuter Hizo, kwani
zilikuwa zinawasaidia katika masoma yao.

Katika Hatua Nyingine Jeshi La Polisi Kwa Kushirikiana Na Askari
Wanyamapori Wamefanikiwa Kumkamata Mtu Mmoja Akiwa Na
Pembe Ya Ndovu Yenye Urefu Wa Sentimeter 90 Na Uzito Wa
Kilogram 3.85 Aliyokuwa Ameliweka Kwenye Mfuko Na Kusafirisha Kwa Kutumia Pikipiki Aina Ya Haojue Yenye No.818btu Rangi
Nyeusi .