NA RACHEL MKUNDAI,
KIBITI
KIBITI
MAMLAKA
ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara kujisajili na kupata
namba ya utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa kuwa inatolewa bure bila malipo
yoyote.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu kwa Mlipakodi
inayoendelea wilayani Kibiti katika mkoa wa Pwani, Mkurugenzi wa Huduma na
Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo
amesema TRA inawakaribisha wafanyabiashara wote ambao hawajajisajili kufika maeneo
maalumu yanayotoa huduma na elimu kwa mlipakodi katika wiki hii ili wasajiliwe
na kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi waweze kufanya biashara zao kwa Uhuru na kulipakodi
stahiki bila usumbufu.

“Tunafanya wiki ya huduma na elimu kwa lengo la kusogeza
huduma karibu na walipakodi na kuwatatulia changamoto zao zinazohusu ulipaji
Kodi” amesema Kayombo.

Aidha, Kayombo ameongeza kuwa mbali na kutoa elimu kwa njia ya
semina na matamasha maofisa wa TRA wanapita madukani kutoa elimu kwa
wafanyabiasha na kuwasajili kupata namba ya utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ili
kuongeza idadi ya walipakodi na kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari miongoni mwa
watanzania.

Amesisitiza kwamba, TRA imejipanga kufanya wiki ya elimu kwa
mikoa miwili miwili kwa mwezi na hivyo amewataka wafanyabiashara wa kutumia
fursa hii kujisajili na kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi na kuhakikisha
cheti wanatundika katika maduka yao katika sehemu inayoonekana.

Hata hivyo, ameongeza kuwa pamoja na kuwa na wiki ya elimu
lakini pia TRA imetenga siku ya Alhamis kila wiki kwa mameneja wa wilaya na
mikoa nchini kote kuwasikiliza wafanyabiashara na kutatua changamoto zao
ili kuchochea ari ya ulipaji kodi kwa hiari.

Wiki ya elimu kwa mlipakodi inafanyika katika mikoa ya Morogoro
na Pwani kuanzia tarehe 11 hadi 17 Novemba, 2019 ambapo wananchi na
wafanyabiashara watapata fursa ya kuelimishwa masuala ya ulipaji kodi

Huduma zinazotolewa katika wiki hii ni usajili wa
wafanyabiashara na utoaji wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi, Ulipiaji wa
kodi ya majengo, elimu ya kodi na kutatua changamoto mbalimbali za walipakodi
ili kuongeza ulipaji kodi kwa hiari.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw.Richard Kayombo (kulia), akimkabidhi Cheti cha Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) Bw. Abdallah Juma, ambaye ni mkazi wa wilaya ya Kibiti mkoani Pwani, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea katika stendi ya Kibiti wilaya humo.
Mkazi wa Kibiti mkoani Pwani, Mahamoud Hemed Mpikage akionesha Cheti cha Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN) cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kukabidhiwa wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea katika stendi ya Kibiti wilaya humo.
Afisa Mtendaji Kata ya Kibiti wilaya ya Kibiti Ramadhani Mtulia akifungua semina ya elimu ya ulipaji kodi iliyofanyika katika stendi ya Kibiti kama sehemu ya wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea wilayani humo.
Elimu ya mlipa kodi ikiendelea kutolewa na wataalamu wa TRA huko Kibiti |