Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe,Tulia Ackson amewataka vijana kuacha kupoteza Muda Mwingikutumia kuchat kwenye Mitandao ya kijamii na badala yake wanatakiwa kuitumia vyema kwa ajili ya kujiletea Maendeleo.
Mhe.Ackson ameyasema hayo jijini Dodoma katika Kongamano la
Mdahalo wa Wanafunzi wa Vyuo vikuu ,mkoani hapa lijulikanalo kama,IBUA lilioandaliwa na mfuko wa Kuendeleza Sekta za kifedha Tanzania,Financial Sector Deeping Trust[FSDT].
Mhe.Ackson amesema changamoto kubwa ambayo ipo kwa vijana wa sasa ni matumizi ya Mitandao vibaya badala ya kuitumia mitandao hiyo katika kuwaletea maendeleo.
“Sisi vijana unakuta anachati asubuhi mpaka jioni na hanufaiki na
chochote ,siku hizi kumekuwa na Mchepuko tu wa kufungua magroup kwenye whasaap ili awe na yey admin,Vijana tumieni simu kama sehemu ya kufungua fursa na si kwa mawasiliano pekee”amesema.
Aidha Mhe.Ackson amesema vijana hawatakiwi kuwa watazamaji tu kwa mambo yanayoendelea bali wanatakiwa kuwa sehemu ya mambo hayo hususan ushiriki wa mambo mbalimbali ya maendeleo huku akiwataka kuwa na malengo ya dhati pindi wanapoanzisha mradi na kusisitiza kuwa jambo la kwanza katika kufanikisha malengo ni kuwa na wazo na kufuatiwa na mtaji.
“Vijana kuwa hawana mitaji lakini kikubwa kinachohitajika ni wazo na sio mtaji,unakopa kwa ajili ya nini?amesema.Katika hatua nyingine Mhe.Ackson amewataka vijana kuacha kubishana na
watu waliofanikiwa na badala yake kuutumia muda wao vyema kuchapa kazi za kuwaletea Maendeleo .
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa Kuendeleza Sekta za kifedha Tanzania[FSDT]Sosthenes Kewe amesema lengo la Mdahalo huo ni kuwaanda vijana kuwa viongozi wazuri katika taasisi za kifedha huku akisema asilimia 86% ya Watanzania Wote wanaishi katika Maeneo yenye huduma za kifedha kila baada ya umbali wa kilometa 5.
Katika Mdahalo huo uliokwenda sambamba na Mada isemayo”Je,Taasisi Za kifedha zina mchango gani katika kumwezesha msichana na Mvulana?Faustine Edward kutoka chuo cha St.John ameibuka kuwa Mshindi
Kongamano la Mdahalo wa vyuo vikuu mkoani Dodoma maarufu IBUKA limekwnda na kaulimbiu isemayo ,Naweza,Nafanya,Nashinda.