Home Mchanganyiko KIKUNDI CHA WAKE WA VIONGOZI CHAKABIDHI MADARASA MANNE NA VYOO KUMI KWA...

KIKUNDI CHA WAKE WA VIONGOZI CHAKABIDHI MADARASA MANNE NA VYOO KUMI KWA KUTUO CHA WATOTO WENYE MAHITAHJI MAALUM CHA BUHANGIJA

0

Mlezi wa Kikundi cha Wake wa Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu , Mama Tunu Pinda (wa tatu kulia) wakiwapa chakula watoto wa kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga baada ya kukabidhi majengo ya vyumba vinne vya madarasa na vyoo kumi, Novemba 10, 2019.

Mlezi wa Kikundi cha Wake wa Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisoma hotuba yake wakati kikundi hicho kilipokabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa Kituo cha waotot wenye ulemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga Novemba 10, 2019. Kushoto ni Mgeni rasmi katika makabidhino hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizindua madarasa manne ya Kituo cha watoto walemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga yaliyojengwa kwa ufadhili wa kikundi cha wake wa viongozi cha New Melleanium Women Group. Wa nne kulia ni Mlezi wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Wapili kulia ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Tunu Pinda, kulia ni Mama Hasina Kawawa, wa tano kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko.

Mlezi wa kikundi cha Wake wa Vingozi cha Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimiana na watoto wa kituo cha walemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga baada ya kikundi hicho kukabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa shule hiyo, Novemba 10, 2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack

Mlezi wa kikundi cha wake wa Vingozi cha New Millennium Group, Mke wa Waziri mkuu, Mama Mary Majaliwa akikumbatiana na Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Mama Tunu Pinda, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu katika hafla ya kukabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa Kituo cha Watoto Walemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga yaliyojengwa kwa ufadhili wa kikundi hicho, Novemba 10, 2019.

 

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

……………….

WAKE wa Viongozi wamesherehekea sikukuu ya Maulid kwa kutoa zawadi ya vitu mbalimbali pamoja na kula chakula cha mchana na watoto wa Kituo cha Watoto Wenye mahitaji maalumn cha Buhangija mjini Shinyanga.

Akinamama hao ambao ni wanachama wa kikundi cha Millenium Women Group, walitoa zawadi hizo jana (Jumapili, Novemba 10, 2019). Zawadi walizozitoa kwa watoto ni pamoja na nguo, sabuni, vinjwaji baridi, madaftari, kalamu na taulo za kike.

Wanawake hao waliongozwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi majengo ya vyumba vinne vya madarasa yaliyojengwa na kikundi hicho pamoja na matundu ya vyoo 10.

  

Baadae wake hao wa viongozi wakiongozwa na Mlezi wao Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na Mwenyekiti wao, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Tunu Pinda walicheza muziki na watoto jambo ambalo liliwafurahisha sana watoto.

Tukio hilo pia lilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko na viongozi wengine wa Chama tawala CCM pamoja na viongozi wa Serikali wa mkoa wa Shinyanga.