Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Singida, Thomas Nyambo (katikati) akifungua kikao cha wadau walioliwezesha zao la alizeti katika mkoa huo kilichoandaliwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima Mkoa wa Singida (SIFACU LTD). Kulia ni Mwenyekiti wa SIFACU LTD, Hamis Rajab na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Faida Mali (Faida Market Link Company) , Tom Sillayo.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Faida Mali (Faida Market Link Company), Tom Sillayo, akizungumza katika kikao hicho.
Wadau wa kilimo cha alizeti wakiwa kwenye kikao hicho.
Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Mkoa wa Singida, Thomas Lijaji akizungumza kwenye kikao hicho namna benki hiyo ilivyoboresha huduma zake, hususani huduma zote za vikundi zinatolewa bure.
Wadau wa kilimo cha alizeti wakiwa kwenye kikao hicho.
Wadau wa kilimo cha alizeti wakiwa kwenye kikao hicho.
Wadau wa kilimo cha alizeti wakiwa kwenye kikao hicho.
Wadau wa kilimo cha alizeti wakiwa kwenye kikao hicho.
Wadau wa kilimo cha alizeti wakiwa kwenye kikao hicho.
Viongozi wakiwa meza kuu.
Wadau kutoka Taasisi za kifedha PASS wakiwa kwenye kikao hicho. Kulia ni Meneja wa Pass-East Central Zone na Busines Development Officer, Meema Meela.
Meneja Mkuu wa SIFACU LTD, Ramadhan Sephu akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea |
Mwenyekiti wa SIFACU LTD, Hamis Rajab, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwakilishi wa Kampuni ya Pyxus, Dickson Kilonzo akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Sillayo aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha wadau na wakulima wa zao la alizeti kilichofanyika jana katika Ukumbi wa Luluma mkoani Singida kwa lengo la kuboresha uzalishaji wa zao hilo. “Kampuni yetu inashirikiana vizuri na serikali hasa ya mkoa wa Singida na kutengeneza mnyororo mzuri, hivyo naiomba serikali iendelee kutoa ushirikiano hata baada ya sisi kumaliza mkataba wetu,mfumo huu uendelee kwa nia ya kuwasaidia wakulima wetu ” alisema Sillayo. Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Mkoa wa Singida, Thomas Lijaji alisema kwa sasa benki hiyo imeboresha huduma zake ambapo vikundi hususani vya wakulima vitakapoenda kufungua akaunti watafungua bure na bila makato yoyote hivyo amewashauri wakulima kuunda vikundi ili iwe rahisi kukopesheka. “Katika kuelekea msimu wa kilimo NBC tumejipanga kwa kuwawezesha wakulima kupata Mikopo itakayowasaidia kufanya shughuli za kilimo, hivyo nitumie fursa hii kuwakaribisha kwenye benki yetu kwa ajili ya kufungua akaunti na kupata mikopo” alisema Lijaji. Awali akifungua kikao hicho Mgeni rasmi ambaye ni Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Singida, Thomas Nyamba aliwataka wadau kutafuta namna ya kuweza kusaidia kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti, huku akivitaka vyama vya ushirika kuwashirikisha wakulima kwa kukaa pamoja . Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Singida (SIFACU LTD) Hamis Rajabu alisema lengo la kikao hicho kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa alizeti ni kuhakikisha uzalishaji wa zao hilo unaongezeka kwa msimu ujao kwani msimu uliopita wakulima walishindwa kuzalisha kwa wingi kutokana na taasisi za kifedha kuchelewesha taratibu za mikopo hadi mwishoni mwa msimu jambo ambalo lilipelekea wakulima kushindwa kuutumia vizuri msimu. Baadhi ya wakulima wa zao hilo wameshukuru kwa mafunzo yanayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali kwa wakulima, na kuiomba serikali kuwawezesha wakulima kupata mitaji itakayowasaidia kuongeza kipato kupitia zao hilo la alizeti. |