Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimuakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mawaziri wa Afya na UKIMWI wa nchi za JUmuiya ya Kiuchumi Kusini mwa Afrika SADC kutembelea Bohari ya Dawa (MSD)
…………………………………………………..
Mawaziri wa Afya na Ukimwi wa Chi za Jumuiya ya Kiuchumi kusini mwa Afrika (SADC) wamefurahishwa na ubora na uwezo wa miundombinu ya kuhifadhia, Kutunza na kusambaza dawa na vifaa tiba wa (MSD)wakati walipotembelea Bohari hiyo jijini Dar es salaam leo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara hiyo kwenye makao makuu ya Bohari ya Dawa (MSD) eneo la Keko. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amesema mawaziri hao wameridhishwa na kiwango cha miundombinu na taratibu za manunuzi za MSD.
Amesema Mawaziri wa Afya wa nchi za (SADC) tayari wamewapa tenda ya manunuzi ya dawa kwa nchi zao ambayo yatafaywa kwa pamoja kulingana mahitaji ya nchi wanachama wa (SADC) watakavyohitaji.
Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa kuagiza dawa kwa pamoja kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kutawapa punguzo kubwa la gharama za manunuzi nchi wanachama wa (SADC) kwakuwa kuagiza dawa kwa pamoja kutashusha bei ukilinganisha na gharama za kuagiza dawa viwandani kwa nchi moja moja.
Mawaziri wa Afya na UKIMWI wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi Kusini mwa Afrika (SADC) wako nchini wa kwa ajili ya kuhudhuria mkutano kusu masuala ya Afya na UKIMWI na kujadili changamoto na mikakati mbalimbali ya kukabiliana na chanagamoto hizo ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali kuhusu afya na Ukimwi.
Mounekano wa Bohari ya Dawa MSD katika maghala ya kuhifadhia dawa yaliyopo Keko jijini Dar es salaam.