Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Sengerema,Denis Luhende jana akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Salum Kalli baada ya hafla ya makabidhiano ya saruji mifuko 26 ya saruji ya kukamilisha ujenzi wa ofisi ya tawi la Katwe.Saruji hiyo ilitolewa na Dk. Bashiru Ally.
Baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya CCM tawi la Katwe wakiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli, wa nne kutoka kushoto mbele ya jengo la tawi hilo.Wa tano kutoka kulia ni Mwenyekiti wa tawi hilo, Ruben Mchembe.
……………………………………………
NA BALTAZAR MASHAKA, SENGEREMA
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Katwe wilayani Sengerema, wamesema uongozi wa Chama taifa umedhihirisha kuwa wa vitendo baada ya Dk. Bashiru Ally kutekeleza ahadi ya mtangulizi wake, Abdurahman Kinana.
Wamesema CCM chini ya Mwenyekiti wake Rais John Magufuli na Katibu Mkuu Dk. Bashiru, wameonyesha kwa vitendo badala ya maneno kutokana na kutekeleza ahadi nyingi zilizoahidiwa kwa wananchi na wana CCM iwe kwa Chama ama serikali.
“Tufikishie salama kwa Mwenyekiti Rais Magufuli tunaridhishwa na utendaji wake lakini pia Dk. Bashiru, ahadi hii ni ya muda mrefu na sasa ameitimiza na inaonyesha CCM na viongozi wake walivyo wa vitendo na si wa maneno.Tunamini jengo letu litakamilika,”alisema Mwenyekiti wa tawi la Katwe, Ruben Mchembe.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Salum, akikabidhi ahadi hiyo ya mifuko 26 ya saruji yenye thamani ya sh.507,000 jana alisema, Kinana (Katibu Mkuu mstaafu) Juni 21, 2015 aliahidi kuchangia sh. 500,000 za ujenzi wa ofisi ya tawi la Katwe wakati akiweka jiwe la msingi.
Alisema hadi anang’atuka hakuwa ametimiza ambapo Agosti Mosi, mwaka huu Dk. Bashiru akiwa ziarani Sengerema katika Jimbo la Buchosa aliahidi kutekeleza kwa asilimia 100 ahadi hiyo ya Kinana, baada ya viongozi wa tawi la Katwe kumueleza wakikumbushia ahadi hiyo ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya Chama.
“Nimekuja hapa kutekeleza ahadi hiyo kwa vitendo ambayo ni mifuko 26 ya saruji kwa maelekezo ya Katibu Mkuu ( Dk. Bashiru) ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Mwanza ili mkamilishe jengo hili.Ahadi hii imetekelezwa kwa asilimia 100,” alisema Kalli akiahidi kuwaletea rangi likamilika walipake na kuonekana la kisasa.
Aidha kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Sengerema, Denis Luhende alipongeza jitihada za wana CCM wa Katwe kujenga ofisi ya Chama na kwa jitihada walizozionyesha wakiungwa mkono na Dk. Bashiru, watawasogea na kulikamilisha jengo hilo.
Naye Katibu wa CCM Kata ya Katwe, Francis Mahuma, aliahidi kuwa watasaimamia kwa dhati ujenzi wa mradi huo na kwamba bado wana changamoto ya samani za ofisi na siyo rangi tu.
“Kwa niaba ya wananchi na wana CCM wa Katwe,tunaamini jengo letu kwa mchango huu sasa litakamilika na hivyo tufikishie salamu na shukurani zetu kwa Dk. Bashiru kuwa alichotoa tumekipokea,”alisema