Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Josephat Kandege akizungumza katika Kongamano Wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga katika wilaya ya Kigamboni ambao sasa wataanza kufurahia mikopo kwa ajili ya kukuza na kuboresha biashara zao kupitia uwezeshaji unatolewa na Benki ya CRDB kupitia mkopo wa ‘Jiwezeshe’ lililofanyikaKibada Kigamboni jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela akizungumza katika kongamano la Wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga katika wilaya ya Kigamboni ambao sasa wataanza kufurahia mikopo kwa ajili ya kukuza na kuboresha biashara zao kupitia uwezeshaji unatolewa na Benki ya CRDB kupitia mkopo wa ‘Jiwezeshe’
……………………………………………..
Wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga katika wilaya ya Kigamboni sasa kuanza kufurahia mikopo kwa ajili ya kukuza na kuboresha biashara zao kupitia uwezeshaji unatolewa na Benki ya CRDB kupitia mkopo wa ‘Jiwezeshe’.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hiyo ya ‘Jiwezeshe’, Nainu Waziri Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Japhet Kandege aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa Benki ya kwanza nchini kuitikia wito uliofanywa na Mheshimiwa Rais wa kuwawezesha wajasirimali wadogo maarafu kama wamachinga ambao wengi wao ni vijana.
“Ni fahari sasa kuona vitambulisho vya Magufuli, vikizidi kuleta neema kwa wajasiriamali wetu wamamchinga kupitia mikopo hii ya ‘Jiwezeshe’ kutoka Benki yetu ya CRDB. Salamu hizi mlizotuletea Benki ya CRDB tutazifikisha kwa Mheshimiwa Rais kumueleza namna ambavyo mmemuunga mkono,” alisema Naibu Waziri Kandege.
Kwa upande wake, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Benard Kibesse aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa Benki ya kwanza nchini kutoa mikopo kwa wajasiliamari wadogo bila riba. “CRDB mmeomyesha njia kuwa hili linawezekana. Mwaka huu mmeanza na wajasiliamari 3,000, nawapa changamoto kuwa mwakani tukikutana kama hivi, muwe mmeshatoa mikopo kwa wajasiliamari 10,000” alisema Dkt.Kibese.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema mikopo hiyo ya ‘Jiwezeshe’ inatolewa kidijitali kupitia huduma ya SimAccount ambapo wateja wataweza kukopa kuanzia kiasi cha shilingi 10,000 hadi shilingi 500,000 kupitia simu zao za mkononi.
“Mjasiriamali anatakiwa kufungua SimAccount kwa kupiga *150*62# na kisha kujisajili kutumia kitambulisho chake cha ujasiriamli, ambapo ataweza kunufaika na mkopo binafsi wa ‘Jiwezeshe’ au kupitia kikundi,” aliongezea Nsekela.
Nsekela alisema kwa kuzingatia mazingira ya biashara za wajasiriamali wamachinga, Benki ya CRDB imeachana na mpango wa kutoza riba kwa asilimia na badala yake mteja atatozwa kiwango kidogo cha kati ya shilingi 5,00 na 2,000 tu pindi arejeshapo mkopo.
“Tumefanya hivi ili kuwapunguzia mzigo wajasiriamali hawa wadogo, ili waweze kuwekeza zaidi faidi wanayoipata kupitia mikopo hii ya ‘Jiwezeshe’,” alisema Nsekela.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri aliwahamasisha wajasiriamali wadogo katika wilaya hiyo kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo ya ‘Jiwezeshe’ kwa kujiunga na huduma ya SimAccount ya Benki ya CRDB.
Kupata maelezo zaidi juu ya mikopo ya ‘Jiwezeshe’ tembelea www.crdbbank.co.tz
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dkt . Bernald Kibese akifafanua jambo kuhusu usimamizi wa benki hiyo kwa taasisi za kifedha.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza katika kongamano hilo .
Baadhi ya watoa mada na wafanyakazi wa benki ya CRDB wakiwa katika kongamano hilo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Josephat Kandege, Mkurugenzi Mtendaji wa (CRDB) Bw. Abdulmajid Nsekela na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh. Sara Msafiri wakisaini vitabu vya wageni.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Josephat Kandege kushoto, Mkurugenzi Mtendaji wa (CRDB) Bw. Abdulmajid Nsekela katikati na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BpT) Dkt. Bernald Kibese wakisaini nyaraka mbalimbali kabla ya uzinduzi wa mikopo hiyo.
Baadhi ya wajasiriamali wakionesha na kuuza bidhaa zao katika kongamano hilo.
Baadhi ya wajasiriamali wakijisajili na akaunti ya JIWEZESHE ya CRDB.
Baadhi ya wajasiriamali wakiserebuka na muziki katika kongamano hilo.
Mwanamuziki Zuena Mohamed maarufu kama Shilole Shishi Baby akiwapa maneno wanawake wajasiriamali waliohudhuria katika kongamano hilo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii. Jinsia. Wazee na Watoto Mh. Dkt. Faustine Ndugulile akiwahutubia wajasiriamali kutoka katika jimbo lake la Kigamboni.
Profesa Andrew Temu kutoka Diligent Consulting Limited akitoa mada katika kongamano hilo.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh. Sara Msafiri akizungumza na wananchi akina mama na akina baba wajasiriamali katika kongamano hilo.
Shilole Shishi Baby akitumbuiza pamoja na akina mama wajasiriamali katika kongamano hilo.
Meneja Uhusiano wa benki ya CRDB , Godwin Semunyu pamoja na baadhi ya Maafisa wa benki hiyo wakiwa wameketi na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kigamboni kwenye kongamano hilo la wajasiriamali.
Picha ya pamoja.