************************************
Nteghenjwa Hosseah, Iringa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo ameelekeza Kamati za Rufaa za Uchaguzi kutofungwa na
maamuzi yaliyofanywa na Wasimamizi/wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi
katika maeneo yao.
Jafo ameyasema hayo Mkoani Iringa wakati wa muendelelezo wa ziara
yake Mikoani kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
unaotarajiwa kufanyika Tar 21/11/2019.
Katika kikao hicho na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Kamati ya
Rufaa pamoja wasimamizi wa Uchaguzi ngazi za Wilaya Mhe. Jafo
ameelekeza Kamati za Rufaa kutofungwa na maamuzi yaliyofanywa na
Wasimamizi/Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wakati wa zoezi zima la
Uteuzi.
“Wasimamia wa Uchaguzi wamefanya kwa nafasi yao kwa kadiri
walivyoona inafaa sasa ni wakati wenu kuyachambua na kujiridhisha na
kazi waliyoifanya maamuzi yao sio ya mwisho ninyi ndio mnatakiwa mtoe
maamuzi ya mwisho katika malalamiko yatakayowasilishwa” Alisema Jafo
Nimelisema hili na naendelea kusisitiza nendeni mkafanye kazi kwa weledi
na mkazingatie haki mkamalize malalamiko yote yatakayowasilishwa
kwenu ili wagombea wawe na amani na Uchaguzi ufanyike salama
alisisitiza Jafo.
“Rufaa iwe rufaa kweli kweli yaan mlalamikaji akifikisha malalamiko yake
kwenu apate suluhisho la malalamiko yake, fanyeni maamuzi yenu kwa
kuzingatia haki” Alisema Jafo.
Aliongeza kuwa msiwe na mashaka katika kazi yenu, mjiamini na
mkatende kwa weledi, mkapitie malalamiko yote kwa makini mkiona mtu
anastahili mrudisheni kwenye kinyang’anyiro msifumgwe na maamuzi ya wasimamizi angalieni uhalisia wa malalamiko anayestahili mpeni na asiyestahili msimpe.
Wakato huo huo Waziri Jafo aliitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama
kuhakikisha wanalinda amani wakati wote wa Uchaguzi.
Waziri Jafo anaendelea na ziara yake katika Mikoa na Njombe, Morogoro
na Tanga.