Kuhani kutoka Makao Makuu ya Kanisa Halisi la Mungu Baba,New Genesis Original,akionyesha kitabu kiitwacho ‘Tanzania ni Taifa Baba’ kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kitakachozinduliwa siku ya Jumapili Novemba 10 mwaka huu jijini Dodoma
Kuhani kutoka Makao Makuu ya Kanisa Halisi la Mungu Baba,New Genesis Original,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu uzinduzi wa kitabu kiitwacho ‘Tanzania ni Taifa Baba’ kitakachozinduliwa siku ya Jumapili Novemba 10 mwaka huu jijini Dodoma
Msimamizi wa barabara ya jiji la Kanisa hilo, Kuhani Lango Moja la Mafanikio,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu uzinduzi wa kitabu kiitwacho ‘Tanzania ni Taifa Baba’ kitakachozinduliwa siku ya Jumapili Novemba 10 mwaka huu jijini Dodoma kushoto kwake ni Kuhani kutoka Makao Makuu ya Kanisa Halisi la Mungu Baba,New Genesis Original
…………………………….
Na Alex Sonna, Dodoma
KANISA Halisi la Mungu Baba linatarajia kuzindua kitabu kiitwacho ‘Tanzania ni Taifa Baba’ ambacho kinaeleza namna Tanzania ilivyopendelewa na Mungu.
Akizungumza leo Kuhani kutoka Makao Makuu ya Kanisa hilo Dar es salaam, New Genesis Original, amesema uzinduzi huo utafanyika jumapili(Novemba 10, 2019), katika ukumbu wa Kilimani Land mark na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na kisiasa.
Amesema kitabu hicho kinatangaza Tanzania kutokana na kuwa na vivutio mbalimbali ikiwemo Mlima Kilimanjaro.
“Natoa wito kwa watanzania waweze kuhudhuria kuna kitu kikubwa Mungu Baba amelifanyia Taifa hili, mambo ya Mungu baba ni tofauti na mambo ya mwanadamu, mambo ya Mungu baba si rahisi kuelewa bali tunaona tu matokeo kama vile Taifa la Israeli,”amesema
Kiongozi huyo amesema Mungu Baba ameshuka Tanzania kama kitabu cha Yohana 4:23 kinachozungumzia Baba kuabudiwa .
“Tanzania ilikuwa inahesabika ya pili kwa umaskini, sasa ile nchi iliyokuwa inahesabika kuwa maskini imenunua ‘cash’ndege nyingi kwa maana hiyo anayefanya ni Mungu Baba yupo ndani ya Rais(Dk.John Magufuli), ”amesema.
Ameeleza kuwa kila kinachofanywa na viongozi ni Mungu Baba yupo ndani yao na yeyote angepewa nchi asingewe kurudisha elimu bure.
“Sio elimu bure hata barabara zimejengwa Dodoma, Mwanza, Iringa, Tabora, Kigoma, lami zimekata kila mahali, hospitali miradi ya maji imejengwa mingi,”amesema.
Naye, Msimamizi wa barabara ya jiji la Kanisa hilo, Kuhani Lango Moja la Mafanikio, amesema Mungu Baba ni sauti, na ndio aliyeumba na kutamka vitu vyote vikatokea.