Home Mchanganyiko KATIBU MKUU ALAT AZIPA TANO AZAKI

KATIBU MKUU ALAT AZIPA TANO AZAKI

0

Na.Alex Sonna,Dodoma

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Serikali za Mikoa na Tawala za Mitaa (ALAT) Elirehema Kaaya,ametoa pongezi kwa Asasi za Kiraia nchini (Azaki) kwa kusimamia malengo pamoja na juhudi walizijiwekea katika kuwanufaisha wananchi.

Hayo ameyasema wakati wa mkutano wa majadiliano ya wiki ya AZAKI yanayoendelea jijini Dodoma,amesema kuwa hakika Azaki zimekuwa zikifanya kazi nzuri na kubwa kwa kutoa Elimu kwa wananchi pamoja Sekta mbalimbali kwa kuwajengea uwezo.

Bw.Kaaya,amesema kuwa wao kama ALAT wamekuwa wakifanya kazi katika maeneo mbalimbali huku wakikutana moja kwa moja na wananchi wamekuwa  wakiona juhudi zinazofanywa na Azaki  kwa kuunga mkono kazi zinafanywa na Serikali katika kuleta maendeleo nchini.

” Sisi ni wadau wakubwa wa Azaki kwa sababu zinagusa moja kwa moja maisha ya wananchi wetu,jukumu letu ni kuziunganisha  Halmashauri zote 185 na malengo yetu ni kutoa huduma kwa amesisitiza Bw.Kaaya

Amesema kuwa wamekuwa wakifanya kazi kwa ushirikiano na AZAKI kweli zimekuwa zikituonesha mchango mkubwa mno hivyo tumejionea ndani ya miaka mitatu wamechangia Bilioni 236 kwenye uchumi wa Nchi yetu.

Hata hivyo ametoa rai kwa Azaki hizo kujikita zaidi katika kuwajengea wananchi uwezo wa kujitegemea kiuchumi, kujenga  miundombinu ya elimu, afya na kuwawezesha kujikomboa kimaisha kupitia miradi mbalimbali wezeshi ya kibiashara.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imeweka sera ambayo Halmashauri zote nchini zinatenga asilimia 10 za bajeti zao kwa ajili ya makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu hivyo amezitaka Azaki kujikita zaidi katika kuwajengea uwezo makundi hayo ili waweze kufaidika na mikopo hiyo.

” Mimi napenda kuona matokeo, Watu wetu wa kijijini anapenda kuona maji salama, huduma ya afya iliyo bora, nitoe rai kwa Azaki zetu nchini zijikite katika mambo yanayoonekana, tujikite katika mambo yanayogusa maisha ya watu wetu, tusiangalie sana matakwa ya wafadhili wetu bali mahitaji haswa ya wananchi ambao tumeamua kuwafanyia kazi,” Amesema Kaaya.