Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wachezaji wa Timu ya Mpira wa Pete ya TAMISEMI (hawapo pichani) leo wakati wa kuwaaga kabla ya timu hiyo kusafiri kuelekea Visiwani Zanzibar katika Michuano ya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019 inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na timu ya mpira wa pete ya TAMISEMI leo baada ya kuwapa baraka za kwenda kushiriki katika michuano ya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019 inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Pete ya TAMISEMI wakipata baraka kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo leo wakati wa kuwaaga kabla ya timu hiyo kusafiri kuelekea Visiwani Zanzibar katika Michuano ya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019 inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akiwa katika picha na Katibu Mkuu, TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga leo wakati wa kuiaga timu ya mpira wa pete ya TAMISEMI kabla ya timu hiyo kusafiri kuelekea Visiwani Zanzibar katika Michuano ya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019 inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
……………………
Na. Majid Abdulkarim
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo ameitakia kila la heri Timu ya Mpira wa Pete ya TAMISEMI inayokwenda kushiriki michuano ya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019 na kuitaka kurudi na ushindi katika michuano hiyo.
Mhe. Jafo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa kuiaga timu hiyo ambayo inategemea kusafiri kuelekea Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Michuano ya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019 ambayo inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
“Ninaomba muwe na nidhamu kwa kuwa ni jambo la msingi katika kufanikiwa katika michuano hii na kupitia msingi huu mtakuwa mmelinda heshima na nidhamu ya wizara” Amesema Mhe.Jafo
Aidha Mhe.Jafo amesema kuwa ili kufikia malengo ya timu hiyo kurudi na ushindi wa Ligi hiyo ya Mapinduzi Zanzibar 2019 lazima kuheshimu maelekezo ya mwalimu na viongozi wa timu waliyoambatana na timu hiyo ili kufikia malengo ya kupata ushindi.
“Naimani timu yetunibora na tunaweza kufanya vyema kama michuano mingine tunavyo fanya vyema hivyo tukafanye vizuri kwani tunao uwezo wa kupata kikombe cha michuano hiyo” Ameongezea Mhe.Jafo
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamuhanga ameitaka timu hiyo kwenda kushindana na so kushiriki ili kuhakikisha wanarudi na kikombe cha michuano ya Ligi ya Mapinduzi Zanzibar 2019.
Kwa kuongezea Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa anatoashukrani za dhati kwa wachezaji na viongozi wa timu hiyo kwa juhudi na mafanikio wanayopata katika kuitumikia timu hiyo na kuwatakia kila la kheri katika safari yao na michuano wanayokwenda kushiriki huko visiwani Zanzibar.