Daktari Marko Hingi akionesha dawa ya nguvu za kiume ya Ujana iliyosajiliwa na baraza la Tiba Aisili na Tiba Mbadala katika maonesho ya kutano wa Mawaziri wa Afya na Ukimwi wa nchi za SADC unaofanyika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.
Daktari Marko Hingi akimuonesha dawa Dkt. Daud Ole Mkopi Ofisa Mipango Mwandamizi Taasisi ya Benjamin William Mkapa aliyefika katika baraza la Tiba Aisili na Tiba Mbadala katika maonesho ya kutano wa Mawaziri wa Afya na Ukimwi wa nchi za SADC unaofanyika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.
Baraza la Taifa la Tiba Asili na Tiba Mbadala limesema tayari limeshasajili dawa 13 zikiwemo za Kisukari, Mifupa, Dawa ya kusaidia akina mama katika masuala ya Uzazi, ikiwemo dawa ya Nguvu za Kiume ya Ujana iliyotengenezwa na Kampuni ya Shatri Herbals ya jijini Dar es salaam iliyosajiliwa mwaka 2017.
akizungumza na Mtandao wa Fullshangweblog katika banda la maonesho la Baraza hilo yanayofanyika Kando ya Mkutano wa Mawaziri wa Afya na Ukimwi wa nchi za SADC Daktari Marko Hingi amesema Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala linataka dawa zote sipimwe na kusajiliwa ili kuwalinda watumiaji wawe salama wakati wanapozitumia dawa hizo.
Amesema Tanzania nzima, Waganga 2902 wamesajiliwa na vituo 100 hivyo kufikia jumla ya waganga wa tiba asili 22102 na vituo 715 vilivyosajiliwa kote nchini kwa mwaka wa fedha 2017-2018.
Utafiti uliofanywa na shirika la Afya Duniani unaonesha aslilimia 60 ya watanzania wanaanza kupata tiba kwa waganga wa kienyeji na baadaye ndiyo hupelekwa hospitali mara wanapougua.
Daktari Marko Hingiamesema Baraza limefanya kazi kubwa ya kuwaelemisha waganga wa jadi juu ya sheria, kanuni na miongozo ya tiba asili na tiba mbadala ili kufanya kazi zao kwa misingi inayoongoza taaluma hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo katika kutekeleza majukumu yao.
Katika maonesho hayo taasisi mbalimbali zinashiriki kwenye mkutano huo zikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, NHIF, Benjamin William Mkapa Foundation, Bohari ya Dawa (MSD) Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) , Baraza la Famasia na nyingine nyingi.