Tamasha la Urithi wa Mtanzania (Urithi Festival 2019) limehitimishwa kitaifa jijini Mwanza Novemba 02, 2019 ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyewakilishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla.
Tamasha hilo lenye dhima pia ya kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii Tanzania, limenogeshwa na mashindano mbalimbali ikiwemo ngoma za asili, mitumbwi, kwaya pamoja baiskeli ambapo washindi wamejinyakulia zawadi kedekede.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza kwenye tamasha hilo lililofanyika katika viunga vya Rock City Mall.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akitoa salamu zake kwenye tamasha hilo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akitoa salamu zake kwenye tamasha hilo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Watemi wa Usukuma akitoa salamu kwenye tamasha hilo.
Mgeni rasmi, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akikabidhi zawadi kwa washindi mbalimbali.
Mgeni rasmi, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati), Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (kushoto) wakiwa kwenye kilele cha Tamasha la Urithi 2019.
Mgeni rasmi, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) pamoja na viongozi mbalimbali wakielekea kwenye mabamba ya maonesho kwenye tamasha hilo.
Mgeni rasmi, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwapungia mkono washiriki wa maonesho kwenye tamasha hilo.