Msanii Doreen Mandawa (wa kwanza kushoto akiwa na rafiki yake Kari Glosmaas, Balozi wa Norway nchi Tanzania, Elizabeth Jacobsen, na Prof Anna Tibaijuka siku ya uzinduzi wa onesho liliandaliwa kwa heshima yake Makumbusho ya Taifa.
Wadau waliohudhuria hafla hiyo.
******************************************
Na Mwandishi wetu
Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiano na marafiki wa msaanii maarufu nchini, Bibi Doreen Mandawa wameandaa onesho la sanaa la kumuenzi msanii huyo.
Onesho hilo ambalo limeandaliwa kwa heshima ya msanii huyo mkongwe mweny umri wa miaka 90 linalenga katika kuonesha mchango wa msanii huyo katika tasinia ya sanaa. Lilifunguliwa rasmi Jumatano na litaendelea kuwepo kwa muda wa mwezi mzima.
Mafiki zake msanii huyo, Bw Dag Nissen,na Kari Glomsaas walifunga safari kutoka Norway kwa ajili ya kuja kushuhudia onesho hilo na kumpongeza kwa kutimiza miaka 90 tangu azaliwe.
Msanii huyo ambaye asili yake ni Uingereza (Scotish) amekaa Tanzania zaidi ya miaka 50 ambapo aliolewa na Mtanzania. Onesho hilo lilifunguliwa rasmi siku ya Jumatano (30 Oktoba 2019) litakuwepo kwa Muda wa mwezi mzima katika ukumbi wa King George.
Balozi wa Norway Nchini Tanzania, Mhe. Elizabeth Jacobse alisema sanaa ina nguvu ya ajabu kwa sababu inaweza kuongea katika mioyo ya watu.
Balozi Jacobsen ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa onesho hilo la picha zilizochorwa na Bibi Doreen Mandawa amesema sanaa ina mchango mkubwa katika kuelimisha na
kuibadilisha jamii.
“Nafurahi kuwa sehemu ya sherehe ya kuenzi kazi za sanaa na mchango wake katika jamii” anasema Balaozi Jocobsen.
Amesema Doreen anawakilisha wanawake wanaofanyakazi kwa bidii, hivyo wanawake wanatakiwa kuiga kwa kufanyakazi kwa bidii na weledi wa hali ya juu.
Prof Anna Tibaijuka amesema Doreen Mandawa ni msanii aliyejitoa kwa ajili ya kuelimisha jamii hivyo anatakiwa kuheshimiwa na kuenziwa.
“ Najifunza mengi kutoka kwa Doreen, ni msaani ambaye alijitoa kwa ajili ya kuelimisha watu” anasema Prof.Tibaijuka.
Kazi ya usanii ni kipaji inachukua muda kwa watu kutambua mchango wako hivyo ni fani ambayo inatakiwa uvumili anasema Prof Tibaijuka na kuongeza kuwa wasanii hawatakiwi kukata tama.
Prof Elias Jengo anasema Doreen ni msanii mbunifu ambaye hanakiri vitu bali anatafsiri vitu na kuweka katika sanaa yake ya uchoraji.
“Nimemfahamu Doreen kwa miaka 54 sasa nafurahi kuona kuwa pamoja na umri wa miaka 90 bado anachora,” anasema Prof Jengo.
Doreen alionesha furaha yake kwa jinsi ambavyo Makumbusho ya Taifa na marafiki zake walivyoamua kumpongeza kwa kazi zake za uchoraji nakutimiza miaka 90 tangu kuzaliwa kwake.
“Yaani sijui niseme nini nafurahi kuwaona rafiki zangu nashukuru sana” anasema Doreen ambaye anaonekana kuwa mzee.