Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS), Francis Kiwanga, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu wiki ya Azaki ambayo itaanza Novemba nne hadi nane mwaka huu na itazinduliwa na Mhe. Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa,kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodma.
Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Dodoma, Fatma Tawfiq ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Woman Wake Up,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wiki ya Azaki ambayo itaanza Novemba nne hadi nane mwaka huu na itazinduliwa na Mhe. Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa ,kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodma.
Mwakilishi wa Msajili wa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOS), Charles Komba,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutoa taarifa kuhusu wiki ya Azaki ambayo itaanza Novemba nne hadi nane mwaka huu na itazinduliwa na Mhe. Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa,kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodma.
Mkurugenzi Mtendaji Haki Rasiliamali,Rachel Chagonja,akizungumza na akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu wiki ya Azaki ambayo itaanza Novemba nne hadi nane mwaka huu na itazinduliwa na Mhe. Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa,kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodma.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia
……………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika wiki ya asasi za Kiraia Tanzania [AZAKI] itakayofanyika jijini Dodoma kuanzia Novemba 4 hadi 8 mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Foundation for Civil Society [FCS] BW.Francis Kiwanga amesema wiki ya asasi za kiraia nchini itakutanisha zaidi ya asasi za kiraia 500 kutoka nchi nzima Tanzania bara na visiwani Zanzibar.
Bw.Kiwanga amefafanua kuwa Wiki ya Asasi za Kiraia [AZAKI] itajumuiya Maonesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa na asasi hizo huku lengo likiwa ni kuimarisha ubia kati ya asasi za kiraia na wadau mbalimbali katika kutimiza azma ya kuiletea Tanzania Maendeleo.
“Lengo la kongamano hilo nikuimarisha ubia kati ya asasi za kiraia na wadau mbalimbali katika juhudi za kutimiza azma ya kuileteaTanzanaia maendeleo,” amesema .
Hata hivyo amesema “Kupitia kongamano hili asasi za kiraia
zitafanya majadilianao juu ya kazi zao, kubadilishana uzoefu na kuona ni jinsi ambavyo zinaweza kushirikiana wenyewe kwa wenyewe na wananchi, serikali, bunge, wabia wa Maendeleo na sekta binafsi,” amesema.
Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Dodoma, Fatma Tawfiq ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Woman Wake Up,amewataka wananchi wa kada zote kuhudhuria maonesho hayo ili kufahamu shughuli na umuhimu wa asasi hizo kwa maendeleo ya jamii.
Mhe.Tawfiq amesema kuwa wanapaswa kufahamu kuwa asasi za kiraia si adui wa serikali bali zinapaswa kushirikiana pamoja katika kufitia azma ya kuwahudumia wananchi.
“Kuna dhana kwamba asasi za kiraia hupokea fedha kutoka kwa wafadhili na kuzitumia isivyo, siyo kweli ingawa inawezekana zipo chache zinafanya hivyo na hiyo haimaanishi kuwa asasi zote zinafanya hivyo bali ni udhaifu wa watu au mtu binafsi,” amesisitiza
Mwakilishi wa Msajili wa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOS), Charles Komba,amesema kuwa serikali inatambua umuhimu wa asasi hizo kwani zimekuwa msaidizi mkubwa kwa maendeleo.
Aidha amesema kuwa asasi za kiraia zimesaidia kufikisha huduma katika maeneo ambayo ni nadra kwa serikali kuyafikia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Haki,Rasilimali ,Mafuta ,Madini na Gesi Rachel Chagonja amesema taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kufanya tafiti mbalimbali zinazohusiana na madini,Mafuta na gesi ambapo ni mchango mkubwa kwa serikali Ya Tanzania.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenyeulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Ummy Ndeliyananga, amesema kuwa kwenye wiki hiyo serikali pamoja na wadau wa masuala ya ulemavu watajadili mwenendo wa utoaji fedha za mikopo kwa kundi hilo muhimu.
Hata hivyo amesema kuwa walemavu wanapaswa kupewa mikopo hiyo ya asilimia mbili inayotengwa kwenye halmashauri ili waweze kushiriki kuimarisha uchumi wan chi.
Afisa Uhusiano wa kituo cha sheria na Haki za Binadamu,Legal Human Rights Centre[LHRC] Michael Malya amesema katika wiki hiyo kituo hicho kitajihusisha na utoaji wa huduma za kisheria.
Ikumbukwe kuwa FCS itatoa tuzo za Umahiri wa asasi za kiraia ili
kusheherekea na kutambua ufanisi na michango za taasisi na watu binafisi katika uchocheaji na uimarishaji wa sera ya maendeleo ya nchi.
Zaidi ya asasi za kiraia 15 zikishirikiana na FCS Kuandaa wiki ya
AZAKI ni LHRC,LSF,Save the children, Wajibu Institute,UN
Women,Oxfam,Twaweza,Policy Forum,msichana Initiative,Hakirasilimali, UNA Tanzania, Acountability Tanzania,Sikika,TLS,SHIVYAWATA,na TANGO.
Kaulimbiu wiki ya asasi za Kiraia [AZAKI] Mwaka ,2019 ni ubia kwa Maendeleo ,Ushirikiano kama chachu ya Maendeleo.