Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila (wa pili kushoto) akiwasili katika kongamano la uwezeshaji kwa wakandarasi na wazabuni wa kanda ya nyanda za juu kusini liloandaliwa na Benki ya CRDB. Wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts, Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Toyi Ruvumbangu na Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu, Dennis Mwoleka.
Mbeya, 30 Oktoba, 2019 – Benki ya CRDB imeandaa kongamano maalum la uwezeshaji kibiashara kwa ajili ya Wakandarasi na wadau mbalimbali wa ujenzi wa miradi ya maendeleo nyanda za juu kusini ikihusisha mikoa ya Mbeya, Njombe, Rukwa na Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano la uwezeshaji kwa wakandarasi na wazabuni wa kanda ya nyanda za juu kusini liloandaliwa na Benki ya CRDB. Wengine pichani waliokaa ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Julius Chalya (wa pili kulia) Afisa Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Toyi Ruvumbangu (wa kwanza kushoto) na Meneja wa Kanda ya Nyand`za Juu, Dennis Mwoleka.
Kongamano hilo ambalo limekutanisha wadau mbalimbali wa miradi ya maendeleo ikiwemo makampuni zaidi ya 300 pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali ikiwamo TANROAD, TARURA na TBA, lilifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Albert Chalamila na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya Rungwe Mheshimiwa Julius Chalya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wuu wa wilaya Nyanda za Juu Kusini.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akihutubia katika ufunguzi wa Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini lililoandaliwa na Benki ya CRDB.
Akitoa hotuba yake wakati wa kufungua kongamano hilo, Mheshimiwa Chalamila aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa kongamno hilo ambalo linatizamiwa kuwa kichocheo kikubwa cha miradi ya Maendeleo nchini kupitia fursa mbalimbali za uwezeshaji zinazotolewa na Benki ya CRDB.
“Niwahamasishe ndugu zangu Wakandarasi na Wazabuni wa miradi ya maendeleo katika mikoa yetu ya nyanda za juu kusini kuchangamia fursa hizi za uwezeshaji zinazotolewa na Benki yetu ya CRDB, ili kwa pamoja tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea ya kuimarisha miundombinu yenu laikini pia uchumi wetu,” aliongezea Mheshimiwa Chalamila.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akijibu swali la moja ya Wakandarasi waliohudhuria kongamano hilo.
Akizungumza katika kongamano hilo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts alimhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuwa Benki ya CRDB kupitia kauli mbiu yake ya “Tupo Tayari” imejipanga vilivyo katika kuhakikisha inashirikiana na Serikali kutimiza azma ya ujenzi wa uchumi wa kati unoshamirishwa na viwanda kupitia uwezeshaji wa miradi mbalimbali nchini.
Dokta Witts alisema Benki ya CRDB imejipanga vilivyo kuwahudumia Wakandarasi nchini huku akitaja baadhi ya huduma ikawamo huduma ya dhamana kwa wakandarasi au wazabuni ambao wanatafuta kazi ijulikanayo kama “Bid Guarantee” dhamana za utekelezaji wa miradi “Performance Guarantee” na dhamana za malipo ya awali “Advance Payment Guarantee”.
Dkt. Witts alisema Benki ya CRDB pia imeboresha taratibu zake za utoaji mikopo na hivyo kuwasihi Wakandarasi hao kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo, kufungua akaunti, pamoja na kujiunga na huduma za bima ili kujikinga na majanga yanayoweza kutokea. “Benki ya CRDB ni Benki yenu, na sisi tupo hapa kuwahudumia niwahakikishie tu sisi Tupo Tayari kuwahudumia,” alihitimisha Dkt. Witts.
Meneja
wa Benki ya CRDB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Dennis Mwoleka, akitoa
maelezo juu ya mikakati ambayo benki hiyo imeiweka katika kuwasaidia Wakandarasi na Wazabuni wa kanda hiyo.
wa Benki ya CRDB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Dennis Mwoleka, akitoa
maelezo juu ya mikakati ambayo benki hiyo imeiweka katika kuwasaidia Wakandarasi na Wazabuni wa kanda hiyo.
Wakandarasi na wadau mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo waliipongeza Benki ya CRDB kwa hatua hiyo ya kuwakutanisha wadau wa sekta ya ujenzi nchini huku wakieleza fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB zitakwenda kuleta sura mpya katika utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu nchini.