Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akizungumza na wadau wakati wa ufunguzi wa Mkutano Baina ya Tanesco na Wateja wakubwa wa kanda ya kati wenye lengo ya kuimarisha Sekta ya Nishati Nchini uliofanyika jijini Dodoma leo.
Meneja Mwandamizi Tanesco kanda ya kati Mhandisi Atanas Nangali,akisoma Hotuba kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge wakati wa ufunguzi wa Mkutano Baina ya Tanesco na Wateja wakubwa wa kanda ya kati wenye lengo ya kuimarisha Sekta ya Nishati Nchini
Sehemu ya wadau wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (hayupo pichani ) wakati wa ufunguzi wa Mkutano Baina ya Tanesco na Wateja wakubwa wa kanda ya kati wenye lengo ya kuimarisha Sekta ya Nishati Nchini uliofanyika jijini Dodoma leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akisisitiza jambo kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano Baina ya Tanesco na Wateja wakubwa wa kanda ya kati wenye lengo ya kuimarisha Sekta ya Nishati Nchini uliofanyika jijini Dodoma leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akimsikiliza Meneja Mwandamizi Tanesco kanda ya kati Mhandisi Atanas Nangali,mara baada ya kufungua Mkutano Baina ya Tanesco na Wateja wakubwa wa kanda ya kati wenye lengo ya kuimarisha Sekta ya Nishati Nchini uliofanyika jijini Dodoma leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano Baina ya Tanesco na Wateja wakubwa wa kanda ya kati wenye lengo ya kuimarisha Sekta ya Nishati Nchini uliofanyika jijini Dodoma leo.
Picha Zote na Alex Sonna-Fullshangweblog
………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKUU wa MkOA wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amelitaka Shirika la Umeme nchini (TANESCO) Kanda ya kati kuanzisha kitengo cha huduma ya haraka (fastruck) ili kuondoa vikwazo kwa wawekezaji kupata huduma hiyo.
Agizo hilo amelitoa leo jijini Dodoma wakati wa mkutano wa kujadili changamoto mbalimbali baina ya TANESCO,wawekezaji na wenye viwanda kutoka mikoa ya Kanda ya kati,wenye lengo la kuimarisha sekta ya Nishati Nchini
Dkt Mahenge amesema kuwa pamoja na kuwa Sera zipo wakati mwingine mnapaswa kwenda nje ya box kubuni utaratibu ambao unawawezesha wawekezaji kupata kwa haraka huduma za Umeme ili walete tija katika mkoa na taifa kwa ujumla hasa ukizingatia tunaelekea katika uchumi wa kati wa viwanda.
“Naomba ifike wakati muwe mnaenda nje ya box,lengo ni kujenga wala sio kubomoa,hivyo ni vema kuwapa kipaumbele wawekezaji ili waanze kutoa huduma ya uwekezaji wa viwanda kwa haraka,” amesema Dkt Mahenge.
Aidha Dkt.Mahenge amelitaka Shirika la Tanesco kuboresha huduma za Umeme katika maeneo ya Mpwapwa,Kongwa,Kibaigwa,Narco,Bahi na Chemba ili iwe rahisi wawekezaji kwenda kuwekeza katika maeneo hayo.
”Mkifanya hivyo katika maeneo hayo ambayo yamekuwa yanaleta shida ya umeme mtakuwa mmesaidia kutatua changamoto za wakazi wa maeneo hayo na wawekezaji” amesisitiza Dkt.Mahenge
Hata hivyo Dkt.Mahenge amewapongeza Tanesco mkoa wa Dodoma kutokana na maboresho ya upatikanaji wa umeme yanayofanyika.
Awali Meneja wa TANESCO Kanda ya Kati Mhandisi Atanas Nangali amesema kuwa wamelazimika kuitisha kikao hicho ili kuangalia njia bora ya kuboresha huduma na kufahamu changamoto zinazowakabili katika kulipa madeni,lakini kubwa zaidi ni kuboresha uhusiano.
“Historia ya Shirika letu inaonyesha wenye viwanda na wawekezaji wote wakubwa wamekuwa wakichangia zaidi ya asilimia 50 ya pato la Shirika hivyo kikao hiki ni muhimu kuangalia bora ya kuboresha mahusiano kati yetu na wateja,” amesema Nangali.
Hata hivyo Mhandisi Nangali,amesema kuwa katika kuboresha miundombinu Tanesco Kanda ya kati inayohudumia mikoa ya Morogoro,Singida na Dodoma imeanza kufanya utanuzi wa kituo cha kupoza Umeme cha Dodoma kutoka uwezo wa sasa Megawati 48 hadi kufikia Megawati 400.
Mhandisi Nangali amesema kuwa miradi mingine ni kituo kipya cha kupiga Umeme kilichopo Ifakara mkoani Morogoro, ambacho kutakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawatts 16 na kituo kile cha singida kitakachoongezewa uwezo kutoka megawatts 32 hadi 400.