Mwenyekiti wa TSA, Imani Dominic akichumpa kuzindua bwawa la kisasa la kuogelea la IST
Waogeleaji wakichumpa wakati wa mashindano ya Taifa ya kuogelea
Mkurugenzi wa IST, Mark Hardeman akizungumza wakati wa uzinduzi
Viongozi wa IST, TSA na waogeleaji wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi
Waogeleaji wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushinda medali mbalimbali
………………
Dar es Salaam.
Klabu ya Taliss-IST imeshinda ubingwa wa mashindano ya wazi ya kuogelea baada ya kukusanya pointi nyingi kushinda timu nyingine saba.
Katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye bwawa la kisasa la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika(IST) Masaki, Klabu hiyo likusanya jumla ya pointi 2,207.
Klabu ya Bluefins chini ya kocha na muasisi Rahim Alidina imeshinda nafasi ya pili kwa kupata pointi 1,281 wakati Klabu ya Morogoro, Mis Piranhas ilishika nafasi ya tatu kwa kupata pointi 830.
Klabu ya Dar es Salaam Swimming Club (DSC) ilimaliza katika nafasi ya nne kwa kupata pointi
- Waogeleaji wa kike wa klabu hiyo walikusanya pointi 373 na wanaume walikusanya pointi 377.
Nafasi ya tano ilikwenda Mwanza ambao walipata pointi 468 huku FK Blue Marlins iliskinda nafasi ya sita kwa kupata pointi 429 na Uwcea Moshi Kilimanjaro ikikusanya pointi 325 na Champion Rise katika nafasi ya nane kwa kupata pointi 244.
Meneja wa timu ya Taliss-IST, Hadija Shebe aliwapongeza waogeleaji wake kwa ushindi huo.
“Ushindi huu ni faraja kwetu na umetokana na juhudi na ushirikiano baina ya makocha, wazazi, wadau na waogeleaji kwa ujumla,” alisema Hadija.