******************
Na Mwandishi wetu-MAELEZO
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa amehimiza mjadala wenye tija kutoka Jumuiya ya Kimataifa ili kuiondolea vikwazo vya kiuchumi nchi ya Zimbambwe.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo katika Mkutano wa 18 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) kutoka Afrika na kwingineko duniani uliofanyika Baku, Azerbaijan.
“Uwekwaji wa vikwazo vya kiuchumi kwa nchi ya Zimbambwe unalemaza ukuaji wa uchumi,ufanyaji wa biashara,uwekezaji na ustawi wa watu”Aliongeza Waziri Mkuu Majaliwa.
Hatua hiyo imekuja wakati China ikiunga mkono wazo la Rais Dkt. Magufuli la kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuindolea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi ambapo kupitia Balozi wake hapa nchini Wan Ke aliitaka jumuiya ya kimataifa kuondoa vikwazo hivyo katika kongamano maalum kuhusu vikwazo vya kiuchumi na hatma ya maendeleo ya Afrika lililofanyika Chuo kikuu cha Dar es salaam.