Home Mchanganyiko RC NDIKILO KUZINDUA KESHO ALBAMU YA NYIMBO ZA INJILI ZA MKUU WA...

RC NDIKILO KUZINDUA KESHO ALBAMU YA NYIMBO ZA INJILI ZA MKUU WA POLISI KISARAWE

0

Mratibu wa Tamasha la injili linalokwenda kwa jina la Kipaji change yhamani yangu kwa kibaha saalama  Kadnas Nassir akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na maandalizi ya onyesho hilo ambalo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandis Evarist Ndikilo.(PICHA NA VICTOR MASANGU).

*******************************************

NA VICTOR MASANGU, PWANI

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kesho anatarajia kuzindua tamasha kubwa la dini linalojulikana kwa jina la Kipaji change thamani yangu kwa Kibaha salama ambali pia litaambatana na uzinduzi rasmi wa albamu mpya ya video inayoitwa nilipigwa picha ikiwa na nyimbo tisa katika ukumbi wa Filberti bayi uliopo  Wilayani Kibaha.

Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa tamasha hilo Kadnas  Nassir alisema kwamba onyesho hilo limeandaliwa na kwa ushirikiano wa umoja wa makanisa Wilayani Kibaha pamoja na mwimbaji maarufu wa  wa nyimbo za injili Eva Stesheni ambaye pia ni mkuu wa Kituo cha polisi Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani.

“Kwa kweli mpaka sasa maandalizi yote tunashukuru Mungu yanaendelea vizuri kwani mipango yote ambayo tumeipanga inakwenda vizuri na kitu kikubwa siku hiyo kutakuwa na burudani mbali mbali kutoka katika kwanya za Mkoa wa Pwani pamoja na nyingine kutoka Jijini Dar es Salaam sambamba na wasanii wengine wa nyimbo za injili.

Pia alisema kwa lengo la kuandaa tamasha hilo kubwa katika Wilaya ya Kibaha ni kuyakutanisha makanisa mbali mbali kwa ajili ya kuweza kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika novemba 24 mwaka huu pamoja na kuzindua albamu hiyo ya video yenye nyimbo za injili.

Aidha katika hatua nyingine mratibu huyo alibainisha kuwa tamasha hilo lina lengo la kuweza kutoa fursa kwa vijana  mbali mbali wa wilayani Kibaha na mkoa wa Pwani wanaoimba mziki wa injili kuweza kukuza vipaji vyao pamoja na kuonyesha uwezo wao wa kuimba.

Mratibu huyo aliongeza kuwa tamasha hilo pia litapambwa na waimbaji mbali mbali wa nyimbo za injili wakiwemo Joel Lwaga, Jane Miso, Sifael Mwabuka na mtoto wa Yohana Antony, pamoja na kwaya ya Haleluya , KKT Tumbi,Anglikaana.AIC sambamba na kwaya ya RC Tumbi na kuongeza kuwa kiingilio kitakuwa shilingi elfu 50 kwa viti maalumu pamoja na shilingi elfu 5 kwa kawaida na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha tamasha hilo.