Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akiongea na watendaji wa wizara yake katika ukumbi wa bodi ya maji, Bonde la Kati – Singida katika kikao kazi kuhusu masuala ya rasilimali watu ambapo amesisitiza umuhimu wa kufanya kazi kama timu.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akiongea katika kikao kazi ambapo amewataka watendaji kuthamini kazi na majukumu ya watumishi katika maeneo yao ya kazi.
Mkurugenzi wa Utawala, Wizara ya Maji Bw. Barnabas Ndunguru akitoa muongozo wa kikao ambapo pia amewashukuru viongozi kwa kuwaamini watumishi katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali.
Mkurugenzi wa Utawala, Wizara ya Maji Bw. Barnabas Ndunguru akitoa muongozo wa kikao ambapo pia amewashukuru viongozi kwa kuwaamini watumishi katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali.
Sehemu ya watumishi wa sekta ya maji walioshiriki kikao kazi kuhusu rasilimaliwatu katika ukumbi wa bodi ya maji, bonde la kati Singida.
……………….
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo amewataka watendaji katika sekta ya maji kufanya kazi kama timu katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora maji.
Amesema hayo katika kikao kazi kuhusu masuala ya rasilimaliwatu katika sekta ya maji kilichofanyika katika ukumbi wa Bodi ya maji, bonde la kati mjini Singida.
“Kujua idadi na ubora wa wafanyakazi na maeneo wanayofanyia kazi ni muhimu” Prof. Kitila amesema na kuongeza kuwa zoezi la kuangalia masuala ya rasilimaliwatu katika sekta ya maji linafanyika kwa sababu mabadiliko makubwa yamefanyika ikiwamo; kuunganishwa kwa mamlaka ndogo za maji zipatazo 20, wataalam wote wa sekta ya maji kurudishwa katika Wizara ya Maji, mamlaka za maji nchini kutakiwa kuhudumia wananchi na kutekeleza miradi ya maji.
Awali, akiongea katika kikao hicho Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amesisitiza umuhimu wa kutoa tuzo na kuwatambua watumishi wanaofanya kazi vizuri.
Mhandisi Sanga amesema kila mtumishi katika sekta ya maji ana mchango mkubwa hivyo kila mwenye wazo alitoe ili kusaidia katika utekelezaji wa kazi za kila siku, ikiwamo kukwamua miradi ya maji iliyokwama.