Akizungumza wakati wa sherehe hiyo,Nyeriga amewataka walimu wa shule hizo waongeze juhudi na maarifa katika ufundishaji, pamoja na kujiwekea malengo ya kuendelea kufanya vizuri zaidi, ili shule hizo kwenye matokeo ya darasa la saba mwakani 2020 ziingie kwenye kumi bora kitaifa.
Amewapongeza walimu wa shule hizo mbili kwa kufanya vizuri kwenye matokeo hayo ya darasa la saba, licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye shule hizo ikiwemo ubovu wa miundombinu na upungufu wa walimu, lakini wamekuwa na moyo wa kujituma na hatimaye kufaulisha wanafunzi wengi tofauti na miaka ya nyuma.
“Mimi kama afisa elimu taaluma manispaa ya Shinyanga, nawapongeza sana walimu wa shule hizi mbili kwa juhudi ambazo mmezionyesha kwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2019, nawaomba pia muongeze maarifa katika ufundishaji pamoja na kumaliza tatizo la mwanafunzi kutokujua kusoma, kuandika, na kuhesabu, ndipo mtafanikiwa kuingia kumi bora kitaifa 2020,”amesema Nyeriga.
Naye Afisa elimu wa shule maalumu manispaa ya Shinyanga Edward Mdagata, ameipongeza Shule ya msingi Buhangija ambayo inafundisha pia wanafunzi wenye mahitaji maalumu, kwa kufanya vizuri kufaulisha wanafunzi hao kwa asilimia 93,huku akiahidi kutatua changamoto ya upungufu wa walimu uliopo shuleni hapo hasa wenye uhitaji maalumu.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Buhangija Selemani Kipanya, amesema wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba walikuwa 139, wavulana 68 na wasichana 71, ambapo wamefaulu 129 sawa na asilimia 93, ambapo wavulana wakiwa 67 na wasichana 62 na kufanikiwa kushika nafasi ya 13 ngazi ya halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kati ya shule 41 ambapo mwaka jana walikuwa nafasi ya 18.
Pia amesema kwa upande wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu waliofanya mtihani walikuwa 18, wenye ualbino sita ambapo wamefaulu wote, wasioona wanne nao wakifaulu wote, viziwi walikuwa nane ambapo walifaulu watano huku watatu wakifeli.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Ibinzamata Daniel Malwa amesema wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba walikuwa 94, wavulana 46 na wasichana 48, ambapo wamefaulu 92, wavulana 45 na wasichana 47 sawa na asilimia 98, na kufanya kushika nafasi ya Saba manispaa ya Shinyanga kati ya Shule 41 ambapo mwaka jana walikuwa wa nafasi ya 15.
Nao baadhi ya wazazi akiwamo Martha Mahulu, wamewapongeza walimu kwa kufanya vizuri kwenye mitihani hiyo ya darasa la saba, na kubainisha ufaulu wa mwanafunzi ndiyo furaha ya mzazi.
Afisa elimu taaluma manispaa ya Shinyanga Essau Nyeriga akiwapongeza walimu wa Shule za Msingi Buhangija na Ibinzamata kwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la Saba mwaka 2019.
Afisa elimu taaluma manispaa ya Shinyanga Essau Nyeriga, akiwataka walimu wa Shule ya Msingi Buhangija na Ibinzamata kuongeza juhudi na maarifa katika ufundishaji, ili waweze kufikia malengo yao ya kuingia kwenye nafasi ya kumi bora kitaifa.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija Selemani Kipanya akisoma taarifa ya matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwenye shule hiyo, ambapo wamefaulisha kwa asilimia 93.
Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Ibinzamata Daniel Malwa, akitoa taarifa ya matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 kuwa wamefahaulisha kwa asilimia 98.
Afisa elimu wa shule maalumu manispaa ya Shinyanga Edward Mdagata akiipongeza Shule ya Msingi Buhangija kwa kufaulisha vizuri wanafunzi wenye uhitaji maalumu.
Afisa elimu Kata ya Ibinzamata Mackline Shija, akiwapongeza walimu wa shule hizo mbili ya Buhangija na Ibinzamata kwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019.
Mtendaji wa Kata ya Ibinzamata Victor Kajuna ,akiwapongeza walimu wa shule hizo mbili na kuwataka waongeze juhudi katika ufundishaji.
Mwalimu wa taaluma katika Shule ya msingi Buhangija Mohamed Makana, akizungumza kwenye hafla hiyo, ambapo amesema majaribio ya mitihani ya mara kwa mara baina ya wanafunzi wa Shule hizo mbili ndiyo yamefanya ufaulu kuongezeka tofauti na miaka ya nyuma.
Mwalimu wa taaluma katika Shule ya msingi Ibinzamata Elice Ndosa Mohamed, akizungumza kwenye hafla hiyo, anasema majaribio ya mitihani ya mara kwa mara baina ya wanafunzi wa Shule hizo mbili ndio yamefanya ufaulu kuongezeka tofauti na miaka ya nyuma.
Mzazi Martha Mahulu akipongeza juhudi ambazo wamezionyesha walimu wa shule hizo mbili katika ufindishaji wao na hatimaye kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba.
Walimu wakiwa kwenye hafla fupi ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019.
Walimu wakiwa kwenye hafla fupi ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019.
Walimu wakiwa kwenye hafla fupi ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019.
Walimu wakiwa kwenye hafla fupi ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019.
Walimu wakiwa kwenye hafla fupi ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019.
Walimu wakiwa kwenye hafla fupi ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019.
Keki iliyoandaliwa na walimu wa Shule za Buhangija na Ibinzamata manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kujipongeza kufanya vizuri kwenye matokea ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019.
Afisa elimu taaluma mansipaa ya Shinyanga Essau Nyeriga akimlisha Keki Afisa elimu Kata ya Ibinzamata Mackline Shija kutokana na kusimamia elimu vizuri kwenye Kata hiyo na hatimaye kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019.
Afisa elimu taaluma manispaa ya Shinyanga Essau Nyeriga akigawa vyeti kwa walimu waliofanya vizuri kwenye masomo yao na kusababisha shule kupata ufaulu mzuri kwenye matokeo hayo ya darasa la saba.
Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa walimu waliofanya vizuri.
Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa walimu waliofanya vizuri.
Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa walimu waliofanya vizuri.
Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea kwa walimu waliofanya vizuri.
Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog