Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini(TTB) Devotha Mdachi akimkabidhi zawadi ya Fulana Bw. Qu Bo Naibu Mkurugenzi wa Utamaduni na Utalii jijini Hangzhou nchini China mara baada ya mkutano kati ya wafanyabiashara na mawakala katika sekta ya Utalii kati ya Tanzania na China kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam jana.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini(TTB) Devotha Mdachi akizungumza na wafanyabiashara na mawakala katika sekta ya Utalii kati ya China na Tanzania uliofanyika jana kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam.
Mshauri wa Masuala ya Utamaduni wa Ubalozi wa China Nchini, Gao Weiakizungumza katika mkutano huo.
MKURUGENZI wa Bodi ya Utalii nchini(TTB) Devotha Mdachi akiwa pamoja na maofisa mbalimbali kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya washiriki mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
Meneja Mauzo wa Shirika la Ndege ATCL Edward Nkwabi akizungumza katika mkutano huo.
Picha mbalimbali zikionesha washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mjadala.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini(TTB) Devotha Mdachi na Bw. Qu Bo Naibu Mkurugenzi wa Utamaduni na Utalii jijini Hangzhou nchini China wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
……………………………………………..
MKURUGENZI wa Bodi ya Utalii nchini(TTB) Devotha Mdachi amesema nchi ya China inatarajia kuleta jumla ya watalii 10,000 kabla ya mwaka 2020 kutokana na uhusiano uliboreshwa kati ya nchi hizo mbili.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam alisema licha ya utalii pia wamingia makubaliano na kampuni ya Touchroad ya China kwaajili ya kuleta wawekezaji nchini hasa watakaolenga sekta ya utalii.
Mdachi alisema kuwa nchi hiyo imeleta watalii 3,3000 kwa mwaka 2018 na kuwa nchi ya sita kwa kuleta watalii wengi nchini.
“Kama mnavyofahamu mwaka jana bodi ya utalii iliandaa ziara ya utalii nchini China tulikubaliana na kampuni ya Touchroad kuleta watalii ,kampuni hiyo iliahidi kuleta watalii zaidi ya 10,000 Tanzania ifikapo mwaka 2020 .
“Sasa moja ya jukumu walilochukua ni kuhakikisha utalii wa Tanzania unatangazwa huko China na leo tuko hapa kwaajili ya kukutana na wageni wanaotoka katika mtaa wa Hangzhou ni mji mkubwa China inayotoa watalii na kupokea watalii, wataalamu hao wanaotokea wizara ya utalii wako hapa kwaajili ya kushawishi kuingia katika mikataba ya biashara.
“Tumeelezwa watu wa hangzhou wanavyopokea watalii wengi na pia wametuonesha jinsi gani wanavyopokea utalii wa wetu ,Kutokana na ushirikiano hao ameweza kuleta mawakala wa utalii na wawekezaji hasa katika sekta ya malazi,”alisema Mdachi.
Alisema mwezi ujao wanatariji kwenda China ili kukutana na mawakala wa uwekezaji kwaajili ya kuingia mikataba mbalimbali.
“Tunatarajia mwezi ujao ujumbe kutoka Tanzania wataenda China kukutana na mawakala wa utalii na wawekezaji wanaotaka kuwekeza hapa nchini na tutaingia kwenye mikataba iliyokamilia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kampuni ya Touchroad kutoka China He Liehui alisema kuwa wanafurahi kuendelea kushirikiana na Tanzania hivyo watahakikisha utalii wa Tanzania utatangazwa nchini China.
“Nashukuru kwa ushirikino tuliooneshwa na Watanazani ninauhakika watu watakuja kutembelea mbuga za ngorongoro na Serengeti pia tunashirikiana na TTB kuleta watalii nchini hapa na pia tunashirikiana na Air Tanzania kwa kusafirisha watu kutoka china,”alieleza Liehui.
Naye Meneja Mauzo wa Shirika la Ndege ATCL Edward Nkwabi ,alisema kuwa wameingia makubaliano na kampuni hiyo hivyo wameahidi kupata abiria 262 kwa wiki moja kutoka china kwaajili ya utalii.
“Kuna kipindi tulienda roadshow nchini China tukakutana na hii kampuni ya Toucharoad wakasema wao wanauwezo wa kuboresha utalii nje ya nchi kwa kupata abiria 262 kila wiki tukaingia makubaliano na utaratibu umeshaanza kufanyika na sasa tuko utaratibu wa mwisho.
“Na safari Zitaanza mwishoni mwa mwezi Novemba,habari nzuri tunapokea ndege nyingine kubwa ujiowake utafungua safari zingine zitaanza nje ya nchi.