Kylian Mbappe (kulia) akishangilia na Mauro Icardi (kushoto) baada ya kuifungia Paris Saint Germain mabao matatu dakika za 61, 79 na 83 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya wenyeji, Club Brugge kwenye mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Jan Breydel mjini Brugge. Mabao mengine ya PSG yalifungwa na Icardi dakika ya saba na ya 63 PICHA ZAIDI SOMA HAPA
Raheem Sterling akishangilia baada ya kuifungia Manchester City mabao matatu ndani ya dakika ya 11 kuanzia dakika ya 58, 64 na 69 katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Atalanta kwenye mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Etihad. Mabao mengine ya Manchester City yalifungwa na Sergio Aguero dakika ya 34 na 38 la penalti kufuatia Atalanta kutangulia kwa bao la penalti pia lililofungwa na Ruslan Malinovskiy PICHA ZAIDI SOMA HAPA