Mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo ambaye pia ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya akiongea na wanchi wa wilaya hiyo ambapo amewatoa hofu wananchi hao na kusema kuwa wilaya hiyo iko salama wakati wote.
Furaha Mganya Mkazi wa Ifakara ,akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani)
……………………
NA FARIDA SAIDY, MOROGORO
Katika hali isiyo ya kawaida kumeibuka hofu wilayani ya Kilombero mkoani Morogoro,ikielezwa kusababishwa na kukithiri kwa vitisho toka kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa dhidi ya wananchi na baadhi ya waliokuwa viongozi wa kisiasa waliohamia vyama vingine hatua iliyoilazimu serikali kuingilia kati na kutoa tahadhari kwa wanao jihusisha na mchezo huo.
Hata hivyo serikali wilayani humo imewatahadharisha baadhi viongozi wa kisiasa wanaotuhumiwa kutoa kauli za vitisho, kwa wananchi wanaohama kutoka kwenye vyama vyao.
Furaha Mganya ni miongoni mwa wahanga wa vitisho hivyo, ambapo alikuwa Diwani kata ya katindiuka Halmashauri ya Mji wa Ifakara Kwa tiketi ya CHADEMA, kabla ya kujiuzuru nafasi hiyo na kuhamia CCM anasema baada ya kutangaza kuhama chama amekua akifuatiliwa akihojiwa na kutolewa kauli za vitisho.
Kufuataia mkasa huo Serikali ya wilaya ya Kilombero inakiri kuwepo kwa viashiria hivyo ambapo Mkuu wa wilaya hiyo James Ihunyo amewatoa wasiwasi wakazi wa Kilombero, akiwataka kuendelea na shughuli zao bila hofu kwani serikali ipo macho kuhakikisha usalama kwa kila raia.