Home Mchanganyiko VODACOM YATOA MSAADA WA KOMPYUTA ZILIZOUNGANISHWA NA INTANETI KWA SHULE 14 WILAYANI...

VODACOM YATOA MSAADA WA KOMPYUTA ZILIZOUNGANISHWA NA INTANETI KWA SHULE 14 WILAYANI URAMBO,KUKUZA ELIMU YA KIDIGITALI

0

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia akimuelekeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe jinsi mfumo wa Instant Schools unavyofanya kazi, Vodacom Tanzania Foundation imekabidhi kompyuta mpakato, router na kuunganisha intaneti yenye tahamani ya Shilingi 67m kwa shule 24 wilayani Urambo.

……………………….

·        Yaonyesha njia katika maendeleo ya teknolojia ya Kidijitali kupitia mfumo wa  e-learning  

·        Zaidi ya wanafunzi 7,000  kunufaika na msaada huo.

Oktoba 19, 2019 Urambo. Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania Plc, kupitia taasisi yake ya Vodacom Tanzania Foundation leo imetoa msaada wa kompyuta na Kipanga njia (Router) vilivyounganishwa katika intaneti kwa shule 14 za Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora. Msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi 67,634,000 ni sehemu ya mpango endelevu wenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa taarifa muhimu katika sekta ya elimu.

Hii ni sehemu ya ushirikiano wa Vodacom  na mfuko wa pamoja wa huduma za Mawasiliano (UCSAF) wa kutoa elimu shuleni kwa kutumia miundombinu bora ya teknolojia ya mawasiliano ya Vodacom kote nchini . Kupitia ushirikiano huo, jumla ya shule 300 na hasa zilizoko vijijini zitapata kompyuta zilizounganishwa katika intaneti bure.

Akipokea msaada huo, katika shule ya Sekondari Urambo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Isack Aloyce Kamwelwe, alisema msaada huo wa kompyuta ni hatua muhimu kuelekea mchakato wa maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano ya kidijitali.

Maendeleo ya kuelekea kwenye matumizi ya dijitali yanaonesha kuwapo mafanikio kutokana na uwepo wa kompyuta kama hizi katika shule zetu sambamba na kasi ya matumizi ya simu za mkononi nchini,” alisema Waziri Kamwelwe.

“Shule ni mahala pazuri pa kuanzia kufundisha matumizi ya kompyuta katika maisha ya kila siku. Kompyuta zikiwa shuleni hazitatumika kwa wanafunzi pekee kujifunza matumizi yake, lakini pia walimu kutumia kompyuta hizi kupata ujuzi zaidi na kuboresha uwezo wao wa kufundisha. Walimu pia watatumia muda huo kuboresha ujuzi wao ili kwenda sambamba na ulimwengu wa kidijitali na kupata maarifa Zaidi,” aliongeza Mh Kamwelwe.

“Tunaamini kwamba kompyuta hizi ni hatua nyingine katika mchakato wa mabadiliko ya kidijitali. Tunawashukuru Vodacom Tanzania Foundation kwa msaada wao mzuri,” alisema Kamwelwe.

Mkurugenzi wa Vodacom Foundation, bi Rosalynn Mworia, alisema msaada huo ni sehemu ya ajenda ya Vodacom Foundation yenye lengo la kusaidia sekta ya elimu ili kutoa elimu bora na kuhakikisha wanafikia malengo ya millenia na ajenda ya kitaifa kama sehemu ya mradi wa shughuli za kijamii.

“Fursa za kidijitali ni nishati muhimu katika uchumi unaokua, zina matokeo ya haraka katika uchumi na jamii kwa ujumla. Kwa pamoja zinachangia ukuaji wa uchumi, kuongeza mianya ya ajira pia ina mchango mkubwa katika kupunguza umasikini, huku ikitoa mwanya katika kuchochea ukuaji wa sekta muhimu kama vile elimu na afya,” alisema bi Mworia.

Vodacom imeamua kuweka nguvu katika maendeleo kidigitali Tanzania. Ndiyo maana tunajivunia kutoa msaada huu leo ambao unajumuisha kompyuta, rota vyote vikiunganishwa katika mtandao vikiwa na thamani za zaidi ya shilingi milioni 67 katika shule 14 wilayani Urambo ambayo inategemea kuwafikia zaidi ya wanafunzi 7,000, alisema Mworia.

Vodacom imejikita zaidi katika kukuza maendeleo ya kidijitali, mawasiliano na ubunifu nchini. Tunataka kuwasaidia wanafunzi ili waende sambamba na zama hizi za kidijitali tulizomo kwa sasa na kuwashawishi zaidi kutokuwa watumiaji tu, bali kushiriki kikamilifu katika fursa za kidijitali. Tukio la leo ni mwendelezo wa utoaji wa Kompyuta chini ya ushirikiano wa Vodacom Tanzania Foundation na UCSAF kwa shule za Tanzania Bara na Visiwani,” alisema Mworia

Wiki iliyopita, Vodacom ilitoa kompyuta na router zilizounganishwa na intaneti yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 48 kwa shule 10 Mkoani Simiyu.

Kompyuta hizi zitawezesha shule hizo kupata taarifa mbalimbali za elimu kutoka katika mfumo wa kidijitali kupitia katika muundo wa foundation yetu na hivyo kuhamasisha usomaji wa kidijitali.

 

Vodacom imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono maendeleo ya teknolojia  shuleni kupitia mpango wa Instant Schools, ambapo imetoa kompyuta mpakato na za kawaida 75 katika wa shule za sekondari za Kambangwa, Makumbusho, Mtakuja na Kinyerezi.