Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii nchini kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto,Patrick Golwike,akizungumza mara baada ya kushiriki zoezi la ujenzi wa vyumba vya maabara tukio hilo limefanyika katika Shule ya Sekondari Iyumbu iliyopo jijini Dodoma
Afisa Tarafa wa Wilaya Dodoma Neema Nyalege ambaye aliyemwakikisha Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi
,akizungumza mara baada ya kushiriki zoezi la ujenzi wa vyumba vya maabara tukio hilo limefanyika katika Shule ya Sekondari Iyumbu iliyopo jijini Dodoma
Sehemu ya wataalamu wa Maendeleo ya jamii pamoja na wananchi walioshiriki katika zoezi la ujenzi wa vyumba vya maabara tukio hilo limefanyika katika Shule ya Sekondari Iyumbu iliyopo jijini Dodoma
Afisa Tarafa wa Wilaya Dodoma Neema Nyalege ambaye aliyemwakikisha Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambia akiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii nchini kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto,Patrick Golwike wakishiriki katika ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule ya Sekondari Iyumbu.
Sehemu ya wataalamu wa maendeleo ya jamii pamoja na wananchi wakishiriki zoezi la ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule ya Sekondari Iyumbu iliyopo jijni Dodoma
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii nchini kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto,Patrick Golwike,akishiriki atika ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule ya Sekondari Iyumbu.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWE BLOG
……………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wataalamu pamoja na Maafisa wa Maendeleo wa jamii nchini wamefanikiwa kuokoa sh milion 6.5 za ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Iyumbu jijini Dodoma,baada ya kushiriki ujenzi wa kumwaga jamvi katika vyumb hivyo.
Ujenzi huo ambao ulianza Desemba 2018,unatarajia kukamilika mwakani ili wanafunzi waliochukua mchepuo wa Sayansi waanze kuvitumia kwa vitendo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii nchini kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto,Patrick Golwike amesema kuwa kazi ya Maafisa na wataalamu wa Maendeleo ya jamii nchini sio kutoa mikopo tu bali ni kusimamia miradi kwa ufanisi inayotekeelezwa na serikali.
Bw.Golwike amesema kuwa kutokana na hilo amewataka maafisa Maendeleo kutambua wajibu wao ili kuhakikisha miradi ya maemdeleo unafanyika kikamilifu.
“Moja ya kazi za Maafisa Maendeleo ni pamoja kusimamia miradi hivyo ni lazima tuamshe ari kwa wananchi kushiriki katika miradi ya maendeleo,” amesema Golwike.
Amesema kuwa chama cha maafisa maendeleo nchini (CODEPATA)kabla ya mkutano Mkuu waaafisa Maendeleo wameamua kushiriki zoezi hilo ikiwemo kutoa mifuko 120 ya cementi ambayo imesaidia kuweka jamvi katika vyumba hivyo vya madarasa na maabara.
Aidha amesema kuwa lengo lao ni kuona kila mwananchi anatambua umuhimu wa miradi ya maendeleo ambayo inayotekelezwa na wao wanasaidia kuiendeleza.
Kwa upande wakAfisa Tarafa wa Wilaya Dodoma Bi.Neema Nyalege ambaye aliyemwakikisha Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi amewapongeza maafisa maendeleo kutokana na jitihada walioonyesha katika kuchangia Maendeleo kwenye ujenzi huo.
Amesemam kuwa vyumba vya maabara katika sekondari ni muhimu hivyo ni vema wananchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuamka kufanya shughuli za maendeleo hususani za ujenzi wa vyumba vya maabara ambavyo ni muhimu kwa wanafunzi kufanya kazi kwa vitendo
Awali Afisa mtendaji wa Kata ya Iyumbu Vicent Leo amesema kuwa ujenzi huo ulianza Decemba 2018,wakiwa na lengo la kukidhi mahitaji ya wanafunzi katika masomo ya sayansi.
Hata hivyo Bw.Leo amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo utasaidia kupunguza adha ya wanafunzi kutembea kilomita 24 kwa ajili ya kwenda shule ya sekondari Kisasa wakitokea eneo la Iyumbu.
“Tunawashkuru maafisa maendeleo kwa kujitokeza kuchangia ujenzi wa vyumba vya maabara,tunaomba na wengine wafanye hivyo,” amesema Leo.
Hata hivyo amesema kuwa wanaamini pamoja na nguvu kazi ya wananchi wa eneo hilo na wadau mbalimbali wanaojitokeza nyumba hivyo hadi kufikia mwakani vitakuwa vimekamilika.