Home Mchanganyiko GAGUTI AONGOZA KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOANI KAGERA  KUTATUA KERO ZA...

GAGUTI AONGOZA KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOANI KAGERA  KUTATUA KERO ZA WANANCHI

0

Na Silvia Mchurua.
Bukoba.
Bodi ya barabara mkoa wa kagera imeazimia kutatua kero za wananchi katika kikao cha bodi hiyo kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa huo Brigedia General Marko Erisha Gaguti  amewaongoza wajumbe kujadili kero za barabara katika Halmashauri ya Kyerwa, Karagwe, Missenyi, Ngara pamoja na wilaya ya Muleba.
Alizungumza  meneja wa TANROAD kagera Engineer Andrea Kasamwa amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 19/20 serikali imetenga bajeti ya Tsh.bilion 13.7 kati ya hizo bilion 2.7 zatatumika kulipa maboresho ya mwaka uliopita na bilion 10.9 zitatumika mwaka huu, pia mbali na bajeti hiyo amesema zipo fedha za maendeleo bilion 4.9 ikiwa bilion 3.4 zimetoka serikalini na bilion 1.4 zimetoka mfuko wa barabara.
“Barabara zote tumezipa kipaumbele ambazo zina kilomita 1960  kila mwaka lazima zitengenezwe na wakala wa barabara ikiwa barabara zinafanyiwa matengenezo mwaka huu ni Muhtwe kamachumu Muleba pamoja na Muleba Kanyambogo Lubya, vilevile ipo barabara ya Lusumo Lusahunga serikali imetoa pesa maalumu bilion 5 kwa ajili ya kukarabati sehemu kolofi” alisema Engineer Kasamwa.
Ameongeza kuwa kazi zote za maendeleo bodi itaongeza kasi ili kukarabati na pia bodi itaandika andiko kuomba kuongezewa bajeti kwa ajili ya ukarabati wa barabara pia amewaomba wananchi kutunza vizuri miundombinu ya barabara ili kuchochea zaidi juhudi za serikali ya awamu ya tano.
Aidha maadhimio ya ya kikao hicho cha bodi kimeadhimia kuwa barabara ya Kyebitembe iongezewe kasi zaidi mpaka kilomita 10 ambapo adhimio hilo litasimamiwa na mkuu wa mkoa Kagera ambapo pia mkuu wa mkoa ameiomba bodi ya barabara kuzikarabati barabara zilizo kwenye mpango hili kupunguza kero kwa wananchi.
Nae Mb.wa jimbo la Bukoba vijijini  Jasson Rweikiza ameiomba bodi kuitambua Halmashauri ya vijijini kwenye mpango angarau kilometa 5 kutokana na kusaulika kwa mda mrefu ambapo ombi hilo limewekwa kwenye maadhimio 6 yaliyotokana na kikao hicho.
Sambamba na hayo nae Engneer  Avith Theodory  ambae ni meneja Tarura mkoa wa kagera amesema kuwa kutokana na halmashauri ya Bukoba vijijini kusahulika kwa mwaka wa fedha 2019 basi kwa mwaka 2020 itawekwa kwenye mpango kutokana na kuyatambua makao ya Halmashauri hiyo