Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akivishwa skafu na Daniel Ngwema Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Mpira wa Kilimahewa kwa ajili ya kushuhudia fainali ya timu ya Nyakahanga dhidi ya timu ya Magambo katika mashindano ya ligi ya Bashungwa Karagwe Cup iliyofanyika katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo, Mhe.Godfrey Mweruka akiwa pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda, Mhe.Innocent Bashungwa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa ameongozana na Mkuu wa wilaya ya Karagwe, Godfrey Mweruka akisalimiana na wachezaji wa timu Nyakahanga kabla ya mchuano huo kuanza katika uwanja wa Kilimahewa uliopp katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi ya cheti mshangilia bora wa mashindano ya Ligi ya Bashungwa Karagwe Cup kabla kufunga mashindano hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kilimahewa kushuhudia mechi kati ya timu ya Nyakahanga ambayo imeibuka kidedea katika ya timu ya Nyakahanga na Magambo. Wa pili Julia ni Waziri wa Biashara na Viwanda, Mhe.Innocent Bashungwa.
Baadi ya umati wa wakazi wa Karagwe waliojitokeza kushuhudia mechi kati ya Nyakahanga na Magambo ambapo Nyakahanga iliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu( Julia) akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kushuhudia fainali ya mechi kati ya Nyakahanga na Magambo kabla ya kufunga ligi ya mashindano ya mpira wa miguu wa Bashungwa Karagwe Cup.
Vijana wa skauti wakipiga paradi mbele ya mgeni rasmi kabla ya fainali ya Bashungwa Karagwe Cup kuanza.