Home Mchanganyiko MAKATIBU WAKUU WA SADC  KUJADILI  MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UJANGILI

MAKATIBU WAKUU WA SADC  KUJADILI  MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UJANGILI

0

Makatibu Wakuu wa Wizara za Maliasili,Utalii na Mazingira kutoka nchi za SADC wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kufungua mkutano huo

Katibu Mkuu wa Wizara ,Profesa Adolfu Mkenda akifungua mkutano wa makatibu wakuu wa Wizara za Maliasili,Utalii na Mazingira kutoka nchi za SADC.

Mkurugenzi wa idara ya Chakula ,kilimo na Maliasili kutoka Sektretarieti ya SADC ,Domingos Zephania Gove Akizungumza

washiriki wa mkutano

********************************

Makatibu Wakuu kutoka Wizara za Maliasili,Utalii na Mazingira wa nchi za SADC wameanza vikao vya kujadili na kuweka agenda za mkutano wa Mawaziri wa sekta husika kutoka umoja huo ambapo wanatarajia kujadili mpango mkakati wa pamoja wa kukabiliana na ujangili ili kutomokeza ujangili katika nchi mwanachama.

Katibu Mkuu wa Wizara ,Profesa Adolfu Mkenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa makatibu wakuu kutoka nchi mwanachama  amesema kuwa mkutano huo utajadili mambo mbalimbali ikiwemo vita dhidi ya ujangili ambayo inapaswa kuungwa mkono kwa nchi zote mwanachama badala kuachwa kwa nchi moja.

Mkenda amesema kuwa nchi moja ni vigumu kupambana na ujangili hivyo tunahitaji kuunganisha nguvu kwa nchi zote ili ziweze kufanikisha juhudi za kupambana na ujangili.

“Tunahitaji kuwa na mpango mkakati wa kukuza utalii katika nchi za SADC  hii ni moja kati ya ajenda muhimu zitakazojadiliwa” Alisema Profesa Mkenda

Mkurugenzi wa idara ya Chakula ,kilimo na Maliasili kutoka Sektretarieti ya SADC ,Domingos Zephania Gove amesema kuwa wanahitaji kutembea pamoja kama nchi za SADC katika kuweka mikakati katika masuala ya kimazingira,Utalii na Wanyamapori .

Gove amesema kuwa wanahitaji kuthibitisha program za pamoja za kukuza utalii na kusimamia maliasili katika ukanda husika.